Akiwa ameongozana na jopo la wataalamu sambamba na Meya wa Manispaa
hiyo, Amir Nondo, Ntambi alisema ufa ulioripotiwa na unaoonekana katika
daraja hilo ni zege maalumu iliyowekwa kuondoshea maji ya mvua kwa
urahisi.
“Mpasuko huu sio wa daraja ni zege iliyowekwa juu kuinua mgongo, ili
kuondoshea maji ya mvua kwa urahisi…na hili tunaweza kulikwangua
tukaliondoa lote bila kuathiri daraja hili,” alisema Ntambi.
Meya Nondo alisema daraja hilo limejengwa kwa kuzingatia aina zote za
vipimo na ni daraja pekee la mfano mjini humo maalumu kupunguzia
msongamano wa vyombo vya moto kati kati ya mji huo.
“Unajua daraja hili lilivyojengwa limepachikwa hapa juu hata kama
itatokea kupata dhoruba yoyote ni rahisi kuondolewa na kupachikwa
jingine…huu ni mfumo wa kisasa wa kitaalamu katika ujenzi madaraja;
wananchi wawe huru kulitumia,” alisisitiza Nondo.
Hivi karibuni Tanzania Daima ilitoa taarifa ikionyesha hofu ya daraja hilo kukatika ikiwa ni miezi michache tangu kukabidhiwa.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment