Home » » Viwanda hatarishi kufungwa

Viwanda hatarishi kufungwa

KIwanda cha 21st Century MorogoroSERIKALI imetangaza kuvifunga viwanda vinavyohatarisha uhai wa viumbe hai nchini na kumwagiza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, kukifunga Kiwanda cha 21’st Century kikidaiwa kutiririsha maji yenye kemikali ya sumu katika mto Ngerengere.
Kiwanda hicho ambacho awali kilimilikiwa na serikali kabla ya kubinafsishwa mwaka 1998 kilifahamika kwa jina la Morogoro Polyster Textile Limited .
Akifungua mafunzo ya wataalamu wa kuandaa programu ya wizara hiyo waliokutana mjini hapa, Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Magembe, aliitaka ofisi ya mkoa kukifunga kiwanda hicho hadi kitakaporekebisha miundombinu yake.
Profesa Maghembe alisema wakati taifa linahangaika kusogeza huduma ya majisafi na salama jirani na makazi ya watu nchini, haitaweza kuwavumilia na kuwakumbatia wawekezaji wanaohatarisha maisha ya viumbehai.
“Ni kweli serikali inahitaji wawekezaji, lakini sio wanaokiuka mikataba na masharti ya utunzaji wa mazingira…tutafunga viwanda vyote vinavyosababisha uharibifu wa mazingira,” alisema Profesa Magembe.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa