BONANZA la mchezo wa ngumi za ridhaa na kulipwa lililopewa jina la
‘Cheka Boxing Day’ linatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Yohana Pub,
Msamvu, mjini Morogoro, Desemba 27.
Kwa mujibu wa mwandaaji wa bonanza hilo, Andrew Mtabazi, lengo la
kuandaliwa ni kuibua na kuendeleza vipaji vya mabondia chipukizi mkoani
hapa na pia kuthamini mchango wa bondia Francis Cheka katika kuhamasisha
mchezo huo Morogoro.
Mtabazi alisema, siku hiyo kutakuwa na mapambano mbalimbali ya masumbwi yatakayoanza kupigwa majira ya saa 10 jioni.
Alisema mabondia kutoka klabu mbalimbali za mkoani Morogoro watapanda ulingoni kudhihirisha uwezo wao katika mchezo huo.
Aidha, Mtabazi ametoa wito kwa wadau wa michezo kujitokeza kwa wingi
na kudhamini bonanza hilo linalotarajiwa kufanyika kila mwisho wa mwezi.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment