MKUU
wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, amezishauri benki kuweka vipaumbele
katika kutoa huduma za kibenki kwa wafanyabiashara wadogo na
wajasiriamali kwa kufungua matawi mengi ya huduma hizo vijijini.
Mkuu
wa Mkoa alitoa changamoto hiyo hivi karibuni wakati wa hafla ya
ufunguzi wa Tawi la 18 la Benki ya Diamond Trust Tanzania (DTB) lililopo
mkoani hapa.
Alisema,
huduma za kibenki zinahitajika zaidi maeneo ya vijijini ambako wananchi
wengi ni wazalishaji mali na waendeshaji wa biashara ndogo ili waweze
kuhifadhi fedha zao kwa usalama.
Naye
Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Viju Cherian , alisema ufunguzi wa
tawi hilo katika Mkoa wa Morogoro ni uthibitisho wa mafanikio ya lengo
la benki kupanuka kijiografia nchini Tanzania kwa kuwafikia wateja
Watanzania waliowengi katika sehemu za vijijini.
Kwa
mjibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, DTB ina matawi katika Jiji
la Dar es Salaam, Arusha , Mwanza , Zanzibar, Dodoma , Tanga , Mbeya
,Kilimanjaro, Iringa na sasa Morogoro.
Benki
hiyo yenye makao yake makuu jijini Nairobi, ina jumla ya matawi 95
katika nchi nne za Afrika Mashariki , ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda
na Burundi.
Chanzo;Habari Leo
Home »
» RC Moro ashauri benki kufikisha huduma vijijini
0 comments:
Post a Comment