Home » » Bandari ya nchi kavu kujengwa Moro

Bandari ya nchi kavu kujengwa Moro

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Joel Bendera
 
Serikali ya imetenga zaidi ya ekari 500 kwa ajili ya ujenzi wa bandari ya nchi kavu itakayotumika kuhifadhi shehena ya mizigo na makontena baada ya kupakuliwa kwenye meli za mizigo kutoka katika  bandari ya Dar es Salaam.
Hatua hiyo imelenga kusaidia kuongeza kupunguza msongamano katika barabara ya Morogoro kutoka Dar es Salaam na kupunguza gharama kwa wenye viwanda vya Morogoro ili  kupata malighafi na kusafirisha bidhaa zao kwenda nchi za nje kutokana na mkoa huo kuwa njiapanda ya kuelekea mikoa mingine.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, alisema bandari hiyo itajengwa eneo la Nane Nane na kuwa tayari eneo la kiwanja hicho limeshapatikana.

Mkoa huo ulipewa jukumu la kutafuta eneo hilo na tume ya Mipango ambayo pia itagharamia ujenzi huo sambamba na kutafuta mkandarasi.

Alisema kuwa baada ya kupakuliwa mizigo hiyo  itasafirishwa kwa reli ya kati hadi Morogoro kwa ajili ya kuhifadhi na baadaye kusafirishwa kwa  malori  kwenda mikoani na nchi jirani.

Alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa mpango  wa serikali wa miaka mitatu wa taifa kuwa kwenye uchumi wa kati kupitia Mpango Maalumu wa Matokeo ya Haraka Sasa ( BRN)  ili kupunguza msongamano wa magari makubwa katika Jiji la Dar es Salaam.

Aliwaomba wadau wa sekta ya viwanda, usafirishaji na wengine kushirikiana na wataalamu wa ofisi yake ili kuhakikisha eneo hilo linajengwa miundombinu muhimu ya kisasa.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa