Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera
Morogoro. Wasomi nchini, wamehimizwa kujifunza
lugha ya Kichina, ili washiriki katika kukuza uchumi wa nchi kwa
kuzingatia kuwa uchumi wa dunia unategemea sana bidhaa na mchango wa
China kwa sasa.
Rai hiyo ilitolewa juzi na Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro, Joel Bendera, katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu
wa Wilaya ya Morogoro, Saidi Amanzi.
Hotuba hiyo ilisomwa katika uzinduzi wa
ushirikiano wa ufundishaji wa lugha ya Kichina katika Chuo Kikuu cha
Waislamu cha mjini Morogoro.
Bendera aliwaasa wasomi kutumia fursa ya Kichina,
kujifunza kwa bidii na kupanua wigo takaayowawezesha kuwasiliana katika
kufanya biashara kati ya Watanzania na Wachina. Katika uzinduzi wa
ushirikiano huo, Makamu mkuu wa chuo hicho, Profesa Hamza Ngozi, alisema
kuwa ni vyema wanafunzi wakajifuza lugha hiyo na kuitumia kama nyenzo
ya kutafuta maarifa zaidi katika dunia ya utandawazi.
Alisema chuo kikuu hicho ni tatu nchini kuanza
kufundisha lugha ya Kichina, baada ya Chuko Kikuu cha Dar es Salaam na
Chuo Kikuu cha Dodoma.
Wanafunzi wa chuo kikuu hicho walisema ushirikiano huo ni mzuri na upaswa kuigwa na vyuo vikuu vingine.
chanzo;mwananchi
chanzo;mwananchi
0 comments:
Post a Comment