Morogoro.Vijana mkoani hapa wametakiwa kujiunga
na vikundi vya ujasiriamali kuliko kuwa tegemezi katika jamii na
wengine kujiingiza katika makundi maovu ya matumizi ya dawa za kulevya.
Hayo yalisemwa hivi karibuni na Diwani wa Kata ya Kingo, Fidelis Tairo alipokuwa akizungumza na gazeti hili..
Tairo alisema jamii ya sasa imekuwa na vijana
wengi ambao hawapendi kujishughulisha katika uzalishaji , hivyo kujikuta
wakishindwa kuchangia pato la Taifa.
Alisema ni bora vijana wakajiunga katika vikundi
mbalimbali vya Kuweka na Kukopa (Saccos) ili kuweza kuchukua fedha za
mkopo kwa lengo la kuzitumia katika uendeshaji wa biashara ndogondogo.
“Vijana mnatakiwa kujiunga katika vikundi vya
kuweka na kukopa kuliko kuwa tegemezi katika jamii kwakuwa nyinyi
mnategemewa katika uzalishaji na kuongeza pato la taifa, msitumie nguvu
zenu katika kufanya maovu na kuishia jela”alisema
chanzo;mwananchi.
chanzo;mwananchi.
0 comments:
Post a Comment