WASOMI
wa Chuo Kikuu Mz umb e k i l i c h o p o wilayani Mvomero mkoani Morogoro
wamesema kuwa ni vyema Rais akaondolewa kinga ya kushtakiwa pindi anapotuhumiwa
kwa makosa ya rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma
. Hayo
yalibainishwa jana na wanajumuiya hao kwa nyakati wakati wakijadili rasimu ya
katiba kwa mwaka 2013 ambapo Mkurugenzi wa masomo ya shahada ya kwanza chuoni
hapo, Prof George Shumbusho alisema ni vyema rais akapewa kinga kwa masuala ya
kawaida na si masuala ya rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya rasilimali za
umma.
A i d h a w a s o m i h a o wamependekeza Katiba
Mpya, k u r u h u s u u a n z i s hwa j i wa Mahakama ya Rushwa kama ilivyo kwa
Mahakama za Ardhi, biashara na nyingine, ili kutoa nafasi kwa suala hilo
kushughulikiwa kwa mapana zaidi tofauti na hivi sasa.
Pia mwanafunzi wa chuo hicho, Ester Safari alisema
kitendo cha kuwapeleka watuhumiwa wa rushwa katika mahakama za kawaida,
kumesababisha mrundikano wa mashauri mengi kwa waendesha mashtaka na mahakimu.
Aidha walisema kuwa kesi hizo zimeonekana kukosa
nafasi ya kutosha badala yake kuonekana ni masuala ya kisiasa zaidi, hivyo
kupendekeza rushwa kuwa na mahakama yake itakayokuwa na waendesha mashtaka wake
ili kutilia mkazo vita dhidi ya rushwa.
Kwa upande wake Mhadhiri msaidizi Kitivo cha Sheria
chuoni hapo, Dkt. Eliuther Mushi pamoja na mambo mengine, amependekeza suala la
jukumu la usafi wa mazingira kwa kila mtu iwe ni wajibu wa kikatiba ili
kumfanya Mtanzania kuwajibika na usafi katika maeneo yake badala ya kusubiri
kazi hiyo kufanywa na halmashauri.
Aidha Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe,
Taaluma, Prof. Josephat Itika, ameshauri suala la uzalendo kupewa kipaumbele
kikatiba na suala la kujitegemea likatambulika kikatiba, ili kijana tangu utoto
wake ajue suala hilo ni la lazima.
Aidha wachangiaji wengine, Mhadhiri msaidizi wa
chuo hicho, Innocent Mgeta, mwanafunzi, Charles Ntwale na mwezeshaji, Benjamini
Jonas, wamependekeza katiba ijayo yenye Serikali tatu iwe na Rais mmoja wa
muungano na kwa upande wa nchi washirika yaani Zanzibar na Tanganyika kuwe na
mawaziri wakuu ili kupunguza gharama zisizokuwa na lazima.
Hata hivyo wamelitaka suala la ardhi na maziwa
kuwekwa wazi katika katiba ili yatambulike wazi, tofauti na sasa jambo
linapelekea wananchi kushindwa kushirikishwa na kunufaika na rasilimali hizo.
Chanzo: Majira
0 comments:
Post a Comment