Home » » Mchimbaji madini afa kwa kufukiwa na kifusi

Mchimbaji madini afa kwa kufukiwa na kifusi

WATU watatu wamefariki dunia mkoani Morogoro katika matukio tofauti likiwamo la mchimbaji wa madini kufukiwa na kifusi na mwingine kufa baada ya kunywa pombe kali. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, John Laswai alisema mchimbaji wa madini wilayani 

Ulanga, Stephen Benjamin alikufa kwa kuangukiwa ma kifusi cha mchanga wakati akichimba madini.

Alisema tukio hilo lilitokea Septemba 4 mwaka huu mchana, katika Kijiji cha Chituti, Tarafa ya Ruaha wilayani Ulanga mkoani Morogoro.

Kamanda alisema Benjamin alikuwa akichimba madini kwenye shimo lenye urefu wa mita 20. Alisema katika tukio jingine, mkazi wa Kitongoji cha Mamboya, wilayani Gairo, Emmanuel John (20) alifariki dunia katika Kituo cha Afya Gairo wakati akipatiwa matibabu, baada ya kunywa pombe kali kupita kiasi.

Laswai alisema Omary Ally (38), aliuawa kwa kupigwa na mzee wa miaka 62 katika Kijiji cha Mhelule, Tarafa yaMang’ula wilayani Kilombero.

Wakati huo huo, mkazi wa Kunduchi Dar es Salaam, Godfrey Wilson alikamatwa na noti bandia 656 za dola za Marekani .

Kamanda alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi jioni eneo la Kihonda na askari waliokuwa doria.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa