WAKULIMA wadogo nchini, wametakiwa kushiriki kikamilifu katika
uchangiaji wa maoni juu ya Katiba mpya, ili ipatikane Katiba nzuri. Hayo
yalisemwa jana na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, alipokuwa
akifungua maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa
Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA).
Alisema kwamba, wananchi wakiwamo wakulima wadogo, wanatakiwa kuhakikisha wanashiriki katika kuchangia kutoa maoni ya rasimu ya Katiba mpya, itakayolenga wananchi wote na siyo kwa watu wachache.
Sumaye aliwaonya Watanzania kuepukana na kuchagua viongozi wanaotaka kuingia madarakani kwa mazingira ya rushwa, kwani hawataweza kusimamia kikamilifu Katiba ijayo.
Pia, alisisitiza mipango mbalimbali inayolenga kilimo kwa kushirikisha wakulima wadogo, kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa mipango hiyo kwani bila kupata ushiriki wa walengwa, inaweza kuwa kikwazo katika kufikia malengo yaliyokusudiwa.
“Kumekuwa na mipango mingi ya kuendeleza kilimo, lakini bado haijafahamika ni kwa kiasi gani mipango ya nyuma imefanikiwa.
“Hili linatokea kwa sababu ya kutokuwapo kwa tafiti zinazoonyesha ni kwa kiasi gani mipango iliyopita imefanikiwa na ni kwa nini haikufanikiwa,” alisema Sumaye.
Pia, aliwahimiza wakulima kuhakikisha wanazingatia kilimo bora na chenye tija hasa wakizingatia matumizi bora ya teknolojia za kisasa katika kilimo kwa kuwa hadi sasa kilimo kinachoendeshwa nchini ni duni.
Alisema kwamba, suala la kuzingatia usindikaji wa mazao ya kilimo, ni muhimu katika kuongeza thamani ya mazao na kwamba utaratibu huo utasaidia wakulima kuuza mazao kwa bei kubwa na kuzalisha ajira kupitia usindikaji.
Pia alisisitiza migogoro ya wakulima na wafugaji iangaliwe kwa umakini, ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea kutokana na uwepo wa migogoro hiyo.
Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya MVIWATA, Habib Simbamkuti, alisema hatua ya kuanzishwa kwa umoja huo ilitokana na kutokuwa na chombo kimoja cha kuwaunganisha wakulima.
Alisema MVIWATA ilianzishwa mwaka 1993, ikiwa na wanachama 22 lakini kwa sasa ina wanachama 150,000 katika mikoa yote nchini na ina vikundi 100 vya kuweka na kukopa.
Naye Mwakilishi wa Serikali ya Uswis kupitia Ubalozi wake nchini, Joel Kalago, aliwasisitizia wakulima kushiriki kikamilifu katika utoaji wa maoni kwenye Katiba mpya, hatua ambayo itasaidia katika masuala mbalimbali ya kuendeleza sekta ya kilimo.
CHANZO MTANZANIA

0 comments:
Post a Comment