na Ghisa Abby, Morogoro
MWANASHERIA na mtetezi wa haki za
binadamu Mkoa wa Morogoro, Amani Mwaipaja, amesema kutokuwapo kwa usimamizi
mzuri katika mabaraza ya ardhi ya kata kunasababisha kutokea kwa migogoro kati
ya kijiji na kijiji.
Mwaipaja alisema hayo jana
alipozungumza na Tanzania Daima ofisini kwake juu ya migogoro ya ardhi ya mara
kwa mara.
Alisema migogoro hiyo pia
inasababishwa na baadhi ya watendaji wa vijiji na kata wasiowajibika ipasavyo
kwa wananchi.
“Mara nyingi usimimizi mbovu wa
ardhi kuanzia ngazi ya chini ndio chanzo kikuu cha kuibuka kwa migogoro kati ya
wakulima na wafugaji katika Mkoa wa Morogoro na maeneo mengine,” alisema
Mwaipaja.
Aidha, alisema ili kuhakikisha
changamoto hiyo inapatiwa ufumbuzi wa kudumu ni vema serikali ikaweka mfumo
maalumu wa kutoa elimu kwa wananchi juu ya usimamizi na matumizi bora ya ardhi.
Pia aliwaasa wananchi kuepuka kuuziwa ardhi
kiholela bila ya kupatiwa kibali maalumu kutoka kwa maofisa wa ardhi, kwani
kushindwa kufanya hivyo kutachangia kukosa hatimiliki
CHANZO TANZANIA DAIMA GAZETI
0 comments:
Post a Comment