MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Said Amanzi amewataka maofisa watendaji
wa vijiji na kata kutokuwa chanzo cha migogoro baina ya wafugaji na
wakulima. Amesema migogoro hiyo imekuwa ikitokea mara kwa mara katika
wilaya hiyo kutokana na wafugaji kupewa maeneo kinyume na taratibu.
DC alisema migogoro hiyo imekuwa ikisababishwa na baadhi ya watendaji kutoa vibali vya maeneo kwa baadhi ya wafugaji na hivyo kuwapo kwa migogoro isiyomalizika katika wilaya hiyo,hususan katika Kijiji cha Bonye Tarafa ya Bwakila.
Amanzi alisema Wilaya ya Morogoro ni miongoni mwa wilaya zinayoingiliwa na kuvamiwa na wafugaji kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa na ya Kanda ya Ziwa.
Kuvamiwa huko kunatokana na baadhi ya watendaji kuanzia ngazi ya vitongoji,vijiji na kata kuwatokuwa waaminifu kwa kuwaingiza holela, alisema.
Aliwataka wananchi katika maeneo yanayovamiwa kutoa taarifa kwake badala ya kujichukulia hatua mikononi,
Hata hivyo alisema ni vema watendaji wakawashirikisha wananchi katika baadhi ya uamuzi kwa kuitisha mikutano mikuu ya vijiji ili kuondokana na migogoro ambayo imekuwa ikitokea mara kwa mara.
CHANZO GAZETI LA MTANZANIA

0 comments:
Post a Comment