Home » » MAADHIMISHO YA SIKU YA SERIKALI ZA MITAAYAFANA MOROGORO.

MAADHIMISHO YA SIKU YA SERIKALI ZA MITAAYAFANA MOROGORO.




 NAIBU Waziri wa nchi, ofisi ya waziri mkuu-Tamisemi Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa mkoa wa Morogoro wakati wa kufunga sherehe za maadhimisho ya kilele cha siku ya serikali za mitaa zilizofanyika kitaifa mkoa wa Morogoro na kukabidhi zawadi ya vikombe na tunzo kwa washindani katika mashindano mbalimbali.
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akiwa na furaha huku akiwa amenyanya kombe la ubingwa wa mchezo wa netiboli kufuatia Manispaa ya Morogoro kushika nafasi ya kwanza katika mashindano ya kanda za wilaya katika mchezo huo.
 Naibu Waziri Kassim Majaliwa akimkabidhi tunzo mwandishi mpiga picha wa gazeti la Mwan
anchi Morogoro, Juma Mtanda.
Juma Mtanda akiwa na tunzo hiyo mara baada ya kukabidhiwa na naibu waziri Kassim Majaliwa.
 Nahodha wa timu ya soka ya kata ya Boma Naoda Bakari akikabidhiwa kombe la mshindi wa pili katika mashindano ya TIKA CUP 2013.
 Mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amanzi akimpongeza nahidha wa netiboli Manispaa ya Morogoro kwa kutwaa ubingwa wa mchezo huo kwa kushika nafasi ya kwanza.
 Nahodha wa timu ya Gereji Wida Jumanne akikabidhiwa ngao baada ya kushika nafasi ya kwanza na kutwaa ubingwa wa ligi ya TIKA CUP 2013 na Mhe Kassim Majaliwa.
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Jovis Simbeye naye akipokea kombe baada ya banda la halmashauri ya Manispaa kuibuka bingwa katika kilele cha maadhimishi ya sherehe za siku ya serikali za mitaa kitaifa Morogoro zilizofanyika uwanja wa jamhuri.
Naibu waziri Kassim Majliwa (mwenye miwani) na mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera wakifuarahia jambo wakati Meya wa Manispaa ya Morogoro Amir Nondo akikabidhiwa kombe la ubinga wa soka kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Jovis Sembeye katika sherehe hizo.
 


Na Esther Mwimbula, Morogoro. GAZETI la Mwananchi limetunukiwa tunzo ya cheti na Naibu waziri wa nchi, ofisi ya waziri mkuu-Tamisemi, Kassim Majaliwa kutokana na mchango mkubwa katika sherehe za maadhimisho ya sherehe ya sikukuu ya serikali za mitaa 2013 zilizofanyika kitaifa julai mosi uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro. 
Naibu waziri, Kassim Majaliwa alitoa tunzo hiyo kupitia mwandishi mpigapicha, Juma Mtanda kwa niaba ya gazeti la Mwananchi baada ya kutoa mchango mkubwa katika kutangaza na kuhamasisha mashindano ya ligi ya TIKA CUP 2013 iliyokuwa imeshirikisha timu 24 za kata zinazounda Manispaa ya Morogoro kutoka kwa waandaaji wa mashindano hayo mfuko wa taifa ya bima ya afya.
  
Katika mashindano hayo ambayo yana lengo la kuhamasisha wananchi kujiunga katika mfumu wa tiba kwa njia ya kadi kutoka mfuko wa afya ya jamii inayotaka mwananchi kuchangia sh10,000 ili kupata huduma hiyo kwa mwaka katika vituo vya afya na zahanati ndani ya Manispaa ya Morogoro ambapo timu ya Gereji iliibuka mshindi wa kwanza na kata ya Boma ikishika nafasi ya pili huku Konga ikishika nafasi ya tatu. 
“Mfuko wa taifa wa bima ya afya pamoja na Manispaa ya Morogoro inakutunukia cheti cha pongezi kwa ushiriki wako katika kutangaza na kuhamasisha mashindano ya TIKA CUP 2013 kupitia taaluma ya habari” imeeleza hati ya ponezi ya tunzo hiyo. 
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendela na mkuu wa wilaya ya Morogoro, Said Amanzi kwa pamoja walimpongeza mwandishi, Juma Mtanda pamoja na gazeti la Mwananchi kwa mchango wao katika kutangaza ba kuhamasisha mashindano ya TIKA CUP 2013 Manispaa ya Morogoro yaliendesha sambamba na wiki ya maadhimisho ya siku ya serikali za mitaa kwa ofisi ya Manispaa, halmashauri na taasisi mbalimbali kuadhimisha kwa maonyesha mbalimbali ya bidhaa na utendaji wa kazi wa ofisi hizo. 
Mkuu wa waandishi wa habari mkoa wa Morogoro, Venance George aliipongeza mfuko wa taifa ya bima ya afya, Manispaa ya Morogoro kwa kutoa tunzo kwa mwandishi, Juma Mtanda na Mwananchi kiujumla kwa kutambua mchango wa taaluma ya habari kwani kitendo hicho kinachangia na kutoa changamoto kwa vyombo vingine vya habari ikiwemo kuiga mfano huo wa utendaji nzuri wa kazi wa kujituma.


CHANZO JUMA MTANDA BLOG 

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa