Wanamichezo
kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF)
wakipokelewa na wenzao wa NSSF katika bandari ya Dar es Salaam baada ya
kuwasili katika michezo ya tamasha la Pasaka.
Wanamichezo
kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF)
wakipokelewa na wenzao wa NSSF katika bandari ya Dar es Salaam baada ya
kuwasili katika michezo ya tamasha la Pasaka.
Mapokezi.
Mapokezi.
Ofisa wa NSSF, Pili Mogella (kulia), akimkaribisha Ofisa wa ZSSF.
ZSSF wakiwasili bandarini.
Wachezaji wa ZSSF wakiwa ndani ya basi.
Kocha wa timu ya netiboli ya NSSF, Joseph Ngánza akitoa maelekezo kwa wachezaji wake. Kocha wa timu ya ZSSF, Hadia Ahmada, akitoa maelekezo kwa wachezaji wake. Meneja wa Mahusiano na Masoko wa NSSF, Salim Kimaro, akikagua timu ya netiboli ya ZSSF.
Kocha wa timu ya netiboli ya NSSF, Joseph Ngánza akitoa maelekezo kwa wachezaji wake. Kocha wa timu ya ZSSF, Hadia Ahmada, akitoa maelekezo kwa wachezaji wake. Meneja wa Mahusiano na Masoko wa NSSF, Salim Kimaro, akikagua timu ya netiboli ya ZSSF.
Meneja Mahusiano na Masoko wa NSSF, Salim Kimaro akikagua timu ya netiboli ya NSSF.
Kikosi cha timu ya ZSSF.
Mshambuliaji
wa timu ya netiboli ya ZSSF, Mwasiti Vita, akiwa katika harakati za
kufunga huku Amina Jumanne (kushoto), wa NSSF akijaribu kumzuia katika
mchezo wa tamasha la Pasaka uliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini
Morogoro.
Mchezaji wa NSSF, Maliti, akimiliki mpira huku akizongwa na mchezaji wa ZSSF, Yasinta (GD).
Mchezaji wa timu ya netiboli ya NSSF, Fatuma Sule (C), akichuana na mchezaji wa ZSSF, Fatuma Sule (kushoto).
Mchezaji wa timu ya netiboli ya NSSF, Fatuma Sule (C), akimiliki mpira.
Timu ya netiboli ya NSSF wakiwa katika mazoezi.
Meneja
wa Mahusiano na Masoko wa NSSF, Salim Kimaro (kulia), akizungumza na
wachezaji kabla ya kuanza kwa mchezo wa netiboli ya ZSSF.
Timu ya NSSF ikiwa mapumziko.
Mashabiki wa timu ya netiboli ya NSSF.
Wachezaji wa ZSSF wakiwa katika mazoezi
Kocha wa timu ya soka ya NSFF, Sanifu Lazaro.
Zawadi za washindi.
Mshambuliaji wa NSSF, Katunguja, akimtoka Rashid Suleiman wa ZSSF (kulia).
Ally Chuo wa NSSF (chini), akichuana na Rajabu Said wa ZSSF.
Mchezaji wa ZSSF, Seif Hafidh (kulia), akichuana na Said Mwinyi wa NSSF.
Nahodha
wa timu ya netiboli ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Pili Mogella, akipokea kombe la Ubingwa wa michuano ya tamasha la Pasaka
kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa NSSF, Dominick Mbwete
(kushoto), baada ya kuifunga ZSSF magoli 23-19 katika mchezo
ulifanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Kaimu
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF), Dominick Mbwete (kushoto), akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya
soka ya NSSF, Mzee Mfaume, baada ya kuwafunga ZSSF mabao 2-0 katika
mchezo wa tamasha la Pasaka uliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini
Morogoro.
Wachezaji wa timu ya soka ya NSSF wakiwa katika picha ya pamoja.
Kaimu
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF), Dominick Mbwete (kushoto), akipokea zawadi ya mlango kutoka kwa
Kaimu Meneja wa Rasilimali Watu na Utawala wa ZSSF, Abdallah Mbwana.
Maofisa
wa NSSF na wale wa ZSSF wakiwa katika picha ya pamoja katika bandari ya
Dar es Salaam baada ya kumaliza ziara ya michezo ya tamasha la Pasaka.
Maofisa
wa NSSF na wale wa ZSSF wakiwa katika picha ya pamoja katika bandari ya
Dar es Salaam baada ya kumaliza ziara ya michezo ya tamasha la Pasaka.
TIMU
ya soka ya Shirika la Taifa ya Hifadhi ya Jamii (NSSF), imeichapa bila
huruma timu ya soka ya ZSSF 2-0 katika mchezo wa tamasha la Pasaka.
Mchezo
huo ulifanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini
Morogoro kwa kuzikutanisha timu mbili za mashirika ya Hifadhi ya Jamii
ya NSSF na ZSSF ambapo lengo la michizo hiyo ni kuimarisha ushirikiano
na uhusiano baina ya mashirika hayo mawili.
Mchezo
huo uliianza kwa kasi kubwa iliwachukua dakika 4 NSSF kujipatia bao la
kwanza baada ya mwamuzi wa mchezo huo Fikiri Yusuph kutoa Penalti baada
ya beki wa ZSSF kuunawa mpira katika harakati za kuokoa, mshambuliaji wa
NSSF Said Mwinyi aliipiga penalti hiyo na kuipatia timu yake bao la
kwanza.
Kuingia
kwa bao hilo la mapema kuliwafanya ZSSF kucharuka na katika dakika ya
10 nusura wajipatie bao la kusawazisha baada ya shuti kali lililopigwa
na Juma Mbwana kugonga mwamba na kuokolewa na walinzi wa timu ya NSSF.
ZSSF
waliendelea kulisakama lango la NSSF lakini walinzi wa timu ya NSSF
wamkiongozwa na beki wa wa timu hiyo Hemed Kagobe waliweza kuondoa
hatari hizo na kuwapa wakati mgumu washambuliaji wa timu ya ZSSF.
Katika
dakika ya 27 ya mchezo nusura ZSSF wapate bao la kusawazisha lakini
golikipa wa NSSF, Sadick aliweza kuokoa kiki iliyopigwa na Rashid
Suleimani na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.
Time hizo zilirndelea kushambuliana kea zamu hadi mapumziko NSSF ilitoka ikiwa inaongoza 1-0.
Kipindi
cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko ambapo ZSSF
waliwatoa, Hassani Omar, Abasi Yahaya Abasi, Maulid Suleiman na Hamis
Thani na nafsa zao kuchukuliwa na Yusuf Said, Abdulkarim Rajabu, Khamis
Haji na Mohamed haji Khamis.
NSSF
waliwatoa Nassoro Nassor, Ally Chuo, mfungaji wa bao la kwanza Said
Mwinyi, Sadick Jongo na nafasi zao kuchukuliwa na Bakari Becco, Mwinyi
Mzee, Prosper Lyoba na Shaban Enzi.
Mabadiliko
hayo yalibadilisha sura ya mchezo katika dakika ya 82 mshambuliaji wa
timu ya NSSF, Katunguja aliifungia timu ya bao la pili banda ya kupokea
pasi kutoka kwa Mwinyi Mzee aliyeingia kipindi cha pili, kuingia kwa
bao hilo kuliongeza kasi ya mchezo ambapo ZFF walikuja juu wakitaka
kupata bao angalau la kufutia machozia lakini kikwazo kikubwa alikuwa
mlinda mlango wa timu ya NSSF, Sadick ambaye alikuwa nyota ya mchezo kwa
kuokoa mashuti yaliyokuwa yakielekezwa langoni mwake.
Wakati
huohuo katika mchezo wa netiboli timu ya NSSF ilingára vilivyo baada ya
kuichapa ZSSF kwa jumla ya magoli 23-19 na kunyakua kombe la michuano
hiyo kwa mwaka 2018.
Akizungumza
wakati akitoa zawadi kwa washindi wa michezo hiyo Kaimu Mkurugenzi wa
Rasilimali Watu wa NSSF, Dominick Mbwete, alisema kuwa michezo hii
imelenga kujenga ushirikiano baina ya mifuko, kuimarisha uhusiano na
pamoja na kuboresha afya kwa wadu wa michezo kupitia mifuko hiyo.
“Lengo
la mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka kwa kukutanisha
wanamichezo mbalimbali kutoka katika mashirika ya ZSSF na NSSF ambapo
kushiriki kwa pamoja michezo mbalimbali pamoja na kutoa zawadi kwa
wanamichezo vote walioshiriki katika tamasha hilo."
ambapo
mwakani itafanyika mjini Zanzibar na kuandaliwa na ZSSF watakuwa
wenyeji wa michezo hiyo Zanzib imelenga kujenga ushirikiano baina ya
mifuko, kuimarisha ushirikiano baina ya ZSSF na NSSF pia imelenga
kujenga ushirikiano, uhusiano baina ya wafanyakazi kutoka ZSSF pamoja na
NSSF katika kuimarisha ushirikiano.
0 comments:
Post a Comment