Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Rodney Thadeus akizungumza na
Maafisa Habari na Mawasiliano kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya
Morogoro, Manyara, Dodoma, Kilimanjaro na Tanga yaliyofunguliwa jana
jumanne Machi 20, 2018. Mafunzo hayo ya siku nne yamendaliwa na Mradi na
Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirilkiana na Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa mna Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia ufadhili
wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
Mwezeshaji
na Afisa Habari kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Nteghenjwa Hosseah
akiwasilisha mada kuhusu mtindo wa uandishi wa habari katika tovuti
kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Morogoro, Manyara, Dodoma,
Kilimanjaro na Tanga yaliyofunguliwa jana Jumanne Machi 20, 2018.
Mafunzo hayo ya siku nne yamendaliwa na Mradi na Uimarishaji Mifumo ya
Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirilkiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
mna Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada
la Marekani (USAID).
Baadhi
ya washiriki wa mafunzo ya uandishi wa habari za tovuti kutoka katika
Halmashauri na Mikoa ya Morogoro, Manyara, Dodoma, Kilimanjaro na Tanga
wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mafunzo hayo yaliyofunguliwa jana
Jumanne Machi 20, 2018 Mkoani Morogoro. Mafunzo hayo ya siku nne
yamendaliwa na Mradi na Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa
kushirilkiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa mna Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID)
Baadhi
ya washiriki wa mafunzo ya uandishi wa habari za tovuti kutoka katika
Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini wakifuatilia mada mbalimbali
wakati wa mafunzo hayo yaliyofunguliwa jana Jumanne Machi 20, 2018
Mkoani Morogoro. Mafunzo hayo ya siku nne yamendaliwa na Mradi na
Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirilkiana na Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa mna Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia ufadhili
wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
Afisa
Tehama kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro, Alfred
Chali akichangia hoja wakati wa mafunzo ya uandishi wa habari za tovuti
kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Morogoro, Manyara, Dodoma,
Kilimanjaro na Tanga yaliyofunguliwa jana Jumanne Machi 20, 2018.
Mafunzo hayo ya siku nne yamendaliwa na Mradi na Uimarishaji Mifumo ya
Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirilkiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
mna Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada
la Marekani (USAID).
MAAFISA
Habari na Mawasiliano katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa
nchini wametakiwa kuacha kufungia katika makabati na makabrasha taarifa
chanya za utekelezaji wa mikakati, miradi na programu mbalimbali za
Serikali na badala yake watangaze mafanikio hayo kwa umma.
Hayo
yamesemwa jana (Jumanne Machi 20, 2018) Mkoani Morogoro na Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Rodney Thadeus wakati wa ufunguzi
wa mafunzo kuhusu mwongozo wa uandishi wa habari za tovuti kupitia
Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) unaofadhiliwa na
Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
Thadeus
alisema Serikali inatekeleza miradi mikubwa ya maendeleo katika Mikoa
na Halmashauri mbalimbali nchini, hivyo ni wajibu wa Maafisa Habari na
Mawasiliano katika maeneo hayo watangaze mafaniko hayo badala ya
kusubiri maswali na hoja mbalimbali za wananchi wakihoji katika kupata
uelewa kuhusu miradi hiyo.
“Maafisa
Habari, msifungie taarifa katika makabati yenu toeni taarifa kwa Umma,
wananchi wanapenda kufahamu nini kinafanywa na Serikali yao hivyo jukumu
la Afisa Habari ni kupiga picha kuandaa taarifa na wekeni vielelezo
hivyo katika tovuti zenu ili kujibu hoja za wananchi” alisema Thadeus.
Aidha,
alisema ni wajibu wa Maafisa Habari na Mawasiliano kuhakikisha kuwa
wanaweza taarifa mpya kila wakati ili kuhakikisha kuwa zinakidhi
mahitaji ya msingi ya wananchi ambao wamekuwa wakitumia muda mrefu kwa
ajili ya kutafuta huduma mbalimbali zinazotolewa na Serikali katika
maeneo yao ya kazi.
Akifafanua
zaidi alisema Maafisa Habari na Mawasiliano katika Mikoa na Halmashauri
mbalimbali nchini ndiyo wataalamu wa masuala ya Mawasiliano katika
maeneo yao ya kazi, hivyo wana wajibu wa kutoa ushauri kwa viongozi wao
wa kazi kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa mara kwa mara kuhusu hoja
mbalimbali zinazoulizwa na kujitolea majibu kwa wakati.
Aliongeza
kuwa matumizi ya tovuti ndiyo njia ya haraka zaidi ya kurahisisha mfumo
wa utoaji wa habari na taarifa mbalimbali za Halmashaauri na Mikoa,
hivyo ni wajibu wa Maafisa Habari na Mawasiliano kuwa mabalozi ili
kuhakikisha kunakuwepo na daraja la mawasiliano baina ya Serikali na
wananchi katika kupata suluhu ya masuala mbalimbali ikiwemo migogoro
inayotokea mara kwa mara.
Kwa
upande wake, Kiongozi wa Timu ya Utawala Bora kutoka PS3, Dkt. Peter
Kilima alisema uboreshaji wa tovuti ni sehemu muhimu ya utekelezaji wa
dhana halisi ya utawala bora hivyo ni wajibu wa Maafisa Habari na
Mawasiliano katika Mikoa na Halmashauri nchini kuhakikisha kuwa wananchi
wanapata taarifa zinazozingatia muda na mahitaji yaliyopo.
Aliongeza
ni wajibu wa Maafisa Habari na Mawasiliano kuzingatia mafunzo kuhusu
mwongozo wa uandishi wa habari katika tovuti za Serikali katika Mikoa na
Halmashauri mbalimbali nchini kwa kuwa wananchi wana matarajio makubwa
na Serikali yao katika kuwapatia huduma mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment