Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) Dkt. Stephen Nindi akifungua kikao cha wadau cha kukamilisha Rasimu ya mkakati wa kukabiliana na Changamoto za Matumizi Bora ya Ardhi ambayo imeandaliwa kwa kushirikiana na idara mbalimbali za Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali ikiwemo Shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania,Care International na Ujamaa Community Fund Mkoani Morogoro Leo.
Mratibu wa Miradi ya ardhi kutoka shirika la kimataifa la Care Bi. Mary Ndaro akizungumzia ushiriki wa Asasi za Kiraia katika shughuli ya kukamilisha Rasimu ya mkakati wa kukabiliana na Changamoto za Matumizi Bora ya Ardhi
Baadhi ya wadau wakiendelea kuchangia mambo mambo mbalimbali wakati wa mkutano huo
Mwongozaji wa Kikosi kazi Bw. Victor C. Mwita akiendelea kutoa muongozo wa namna ya kuchangia Mawazo mbalimbali wakati wa mkutano huo uliofanyika mjini Morogoro Leo.
Mratibu wa Miradi ya Ardhi kutoka Shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania Bi. Naomi Shadrack akichangia jambo wakati wa mkutano wa Kikosi kazi.
Wachangiaji wakiendelea kutoa mawazo mbalimbali wakati wa mkutano wa kikosi kazi
Mkutano ukiwa unaendelea
Picha zote na Fredy Njeje
0 comments:
Post a Comment