Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mwonekano
wa mguu wa wa mtoto Sheila Bushiri baada ya kusaidiwa na wafanyakazi wa
benki ya NMB Kilosa kufanyiwa upasuaji na kupewa mguu wa bandia.
Baada ya kusaidiwa mguu wa bandia Sheila sasa anaweza kucheza.
Mwonekano
wa mguu wa mtoto Sheila Bushiri kabla ya kusaidiwa na wafanyakazi wa
Benki ya NMB Kilosa kufanyiwa upasuaji na kupewa mguu wa bandia.
Sheila akiwa katika picha na wafanyakazi wa tawi la NMB wilayani
Kilosa, Morogoro ambao ndiyo waliotoa msaada kwa kushirikiana na Mkuu
Kitengo cha Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) kumsaidia mtoto huyo kufanyiwa
upasuaji kwenye hospitali ya CCBRT na kupewa mguu wa bandia ambao kwa
sasa unamwezesha kutembea tofauti na awali.
Mkuu
wa Shule ambayo anasoma Sheila ya Mazinyungu, Kajika Galani (kulia)
akitoa taarifa ya maendeleo ya masomo ya Sheila kwa Meneja Kitengo cha
Uwabikaji (CSR) cha Benki ya NMB, Lilian Kisamba.
Meneja
wa Kitengo cha Uwajibikaji (CSR) cha Benki ya NMB, Lilian Kisamba
akizungumza na wanafunzi wa darasa ambalo Sheila anasoma.
Wafanyakazi
wa Benki ya NMB wilayani Kilosa, Morogoro kwa kushirikiana na Kitengo
cha Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) cha benki hiyo wametoa msaada kwa mtoto
Sheila Bushiri (7) ambaye alizaliwa akiwa mlemavu wa mguu mmoja
kufanyiwa upasuaji na kumnunulia mguu wa bandia ili aweze kutembea kama
watu wengine.
Akizungumza
kuhusu msaada huo, Meneja wa tawi la benki ya NMB KIlosa, Dismas
Prosper alisema walimjua mtoto huyo kupitia Bi. Shalphina Lipinga ambaye
alikwenda ofisini kwao kuomba msaada wa kusaidia watoto wenye uhitaji
na baada ya kuwaonyesha mtoto huyo waliona kuna haja ya kumsaidia.
Alisema
baada ya kumwona wao kama wafanyakazi walichangishana pesa na kutokana
na utaratibu wa benki hiyo kuwa iwapo wafanyakazi wakichangishana pesa
kitengo cha CSR kuwaongezea pesa sawa na kiwango walichotoa
walifanikisha mtoto huyo kufikishwa kwenye hospitali ya CCBRT iliyopo
Dar es Salaam ambapo alipatiwa matibabu.
“Alikuja
ofisini Shalphina kusema kuwa anasaidia watoto ambao hawajiwezi na
katika maongezi alisema kuna mtoto alizaliwa na ulemavu wa mguu mmoja na
anaishi na bibi yake na anampeleka shule kila siku akimbeba mgongoni
hivyo kama kuna mvua hawezi kwenda shule, mimi nikaona hapo kuna shida
kubwa, “Nilipoona picha hana mguu mmoja kama mzazi iliniuma sana,
niliweza kuwasilisha kwa wafanyakazi wenzangu na nilipowauliza nini
tumfanyie wengi walipendekeza baiskeli na tukakubaliana kuchanga,
alipopelekwa CCBRT walishauri apate mguu wa bandia na wafanyakazi wengi
wakalikubali,” alisema Prosper.
Prosper
alisema lengo la wafanyakazi hao kutoa msaada ni kumwona mtoto huyo
akiwa na furaha na kuendelea na masomo yake vizuri na kwasasa wana
mpango wa kuendelea kutoa msaada kwa watu wengine ambao wanahitaji
kupata msaada ili kuendesha shushuli zao za kila siku kama watu wengine
ambao hawana ulemavu.
“Mwisho
wa siku tulifanikiwa kuweka tabasamu kwenye uso wa yule mtoto kwa
kutumia kile kidogo ambacho Mungu ametusajilia tumsaidie na sio kwa yule
mtoto tu tuna malengo ya kuendelea kusaidia wengine ili na wao wapate
tabasamu,” alisema Prosper. Kwa upande wa bibi yake Sheila, Habiba Said
ambaye ndiyo anaishi na mtoto huyo alisema mtoto huyo alizaliwa na
ulemavu huo na akiwa na miezi tisa mama yake alimwacha nyumbani na
kuondoka huku baba wa mtoto akiwa hajulikani.
Alisema
alimlea mpaka anaanza shule lakini alikuwa akikabiliwa na changamoto ya
kutembea jambo ambalo lilisababisha muda mwingine kushindwa kwenda
shule na hata kushiriki michezo na wenzake lakini NMB wamempa msaada
ambao utamsaidia kufanya mambo ambayo alikuwa anashindwa kuyafanya
awali.
“Sheila
alizaliwa vilevile, mama yake alivyomzaa akiwa na miezi tisa aliondoka
na nimemlea kama kawaida baada ya kukua nikampeleka shule kwa kumbeba
mgongoni…nilikutana na mama Joy (Shalphina Lipinga) nikamwelea na
akasema ataongea na NMB watamsaidia, “Mwanzoni alikuwa anapata shida
kutembea lakini kwasasa anaweza kutembea vizuri yeye mwenyewe,
naishukuru NMB kwa msaada huo, alikuwa hachezi na wenzake lakini kwa
sasa hivi anacheza kama kawaida na anakwenda shule mwenyewe na kurudi
vizuri, nawashukuru sana,” alisema Habiba.
Naye
Mkuu wa Shule ambayo anasoma Sheila ya Mazinyungu, Kajika Galani
aliishukuru NMB kwa msaada ambao imetoa kwa mwanafunzi wake Sheila na
kwa shule hiyo kwa kuipatia msaada wa madawati 78 ambao yamesaidia
kumaliza tatizo la madawati shuleni hapo.
“NMB
tunawashukuru sana pindi mtoto nakuja kuandikishwa hapa alikuwa kwenye
mazingira magumu sana bila bibi yake alikuwa hawezi kuja lakini
wafanyakazi wa NMB wamemsaidia na tangu amesaidiwa sijamwona tena bibi
yake na hata akiwa shule anashiriki michezo na wenzake kama kawaida,
“Mmemsaidia sana naamini hata kusoma kwake kutakuwa vizuri pia hata bibi
yake mmemsaidia sana hasa kipindi cha mvua alikuwa lazima awahi
kumchukua lakini sasa atatembea mwenyewe … pia napenda kushukuru kwa
msaada wa madawati 78 ambayo mmetusaidia, asilimia kubwa ya wanafunzi
kwa sasa wanakaa kwenye madawati,” alisema Galani.
0 comments:
Post a Comment