Home » » WANAWAKE WAONYESHWA NJIA KUPATA MIKOPO

WANAWAKE WAONYESHWA NJIA KUPATA MIKOPO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Christina Haule

SERIKALI mkoani Morogoro imewataka wanawake kujiunga kwenye vikundi na kujitokeza kupata mikopo ya riba ya asilimia 10 inayotolewa kwenye halmashauri mbalimbali mkoani hapa ili kujikwamua kiuchumi.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo alisema serikali, katika kuhakikisha inawawezesha wanawake kivitendo, iliamua kutoa mikopo kwa riba ya asilimia 10.
Alisema hadi sasa, jumla ya Sh. milioni 885 zimeshakopeshwa kwa vikundi 71 vya manispaa, ikiwa ni sehemu ya makusanyo ya halmashauri na asilimia tano kutoka serikali kuu.
Chonjo alisema kuna muitikio mdogo hata hivyo wa wanawake kupata mikopo hiyo, jambo ambalo halileti maana thabiti ya kuanzishwa kwa mikopo hiyo.
Chonjo alisema mikopo hiyo ni fursa nzuri hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kukuza uchumi wa viwanda.
Alisema wanawake wanapaswa kuanzisha viwanda vidogo vitakavyokuwa chachu ya kuanzishwa viwanda vikubwa.
Kwa wasichana, mkuu wa wilaya alisema, mikopo hiyo itawafanya kujikita kwenye biashara na kujiepusha na vishawishi vitakavyowafanya kujiingiza kwenye makundi yasiyofaa, ikiwamo ya ukahaba na madawa ya kulevya.
Alisema Halmashauri hulazimika kutoka mikopo na kwamba kiasi cha Sh. milioni sita hadi 15 hutolewa kwa kikundi kimoja cha watu waliothibitishwa kupata mkopo huo kutoka ngazi ya kata.
Hata hivyo, aliwaasa wakopaji kuhakikisha wanarejesha mikopo hiyo kwa wakati ili kuwafanya wenzao kuweza kukopa na kujikwamua kiuchumi.

CHANZO GAZETI LA NIPASHE

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa