Home » » AUDIO - CHAMA CHA MPIRA MOROGORO CHA IPANDISHA MAWENZI LIGI DARAJA LA KWANZA KWA RUSHWA ,SIRI YA KUPANGA MATOKEO YA VUJISHWA .

AUDIO - CHAMA CHA MPIRA MOROGORO CHA IPANDISHA MAWENZI LIGI DARAJA LA KWANZA KWA RUSHWA ,SIRI YA KUPANGA MATOKEO YA VUJISHWA .

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

SEHEMU YA PILI. Kilichotokea katika upangaji matokeo ya ligi daraja la kwanza msimu ulopita na kupelekea Mbao kupata nafasi ya kucheza ligi kuu Tanzania bara,sasa basi kuna tukio jingine kama hilo limetokea tarehe 4 mwezi huu February pale Morogoro.

Uongozi wa juu wa chama cha soka Mkoa wa Morogoro wawakilishi wa timu ya MAWENZI MARKET na wawakilishi wa timu ya SABA SABA zote za pale Morogoro walipanga matokeo.

Walikubaliana SABA SABA akubali kufungwa na MAWENZI ili MAWENZI wapate nafasi ya kupanda daraja la kwanza, SABA SABA waliahidiwa kusaidiwa pindi mechi yao ya mwisho dhidi ya THE MIGHTY ELEPHANT ya SONGEA, kwa vyovyote vile ili waifunge THE MIGHTY ELEPHANT lakini mambo yakawa tofauti.

Sabasaba akafungwa na akashuka daraja kitu ambacho Saba saba wanalalamika wamesalitiwa na sababu wao wamesalitiwa na sasa wameamua kuachia clip ya sauti ambayo inamaongezi yote waliyokuwa wakipanga vipo vipande viwili.

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa