MKUU wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen, amepiga marufuku wananchi
hususani wakulima kutumia nafaka za chakula kutengenezea pombe kwa
ajili ya sherehe za ngoma 'vigodoro', badala yake wahifadhi kwa matumizi
ya chakula katika kaya zao.
Dk Kebwe alipiga marufuku mtumizi ya nafaka za chakula kutengenezea
pombe katika ziara yake aliyoifanya hivi karibuni wilayani Kilosa
kukagua shughuli za maendeleo.
Alisema utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa siku za hivi karibuni
umeonesha kuwepo uwezekano kukosekana mvua za kutosha maeneo mbalimbali
nchini, ukiwemo mkoa wa Morogoro.
Mkuu wa mkoa alitumia fursa hiyo kwenye mikutano ya hadhara ya
wananchi wa vijiji vya Ulaya, Zombo na Kivungu wilayani humo kuwataka
wahifadhi chakula kidogo kinachopatikana, badala ya kukiuza chote na
fedha zake kutumia kucheza ngoma na kupika pombe.
“Agizo hili ni kwa wilaya za mkoa mzima, kuanzia sasa ni marufuku kwa
mwananchi ama mkulima kuuza chakula chake chote kupata fedha za
kuchezea ngoma na kutengeneza pombe, wale watakaobainika wachukuliwe
hatua za kisheria," alisema.
Alisema hali ya mvua si nzuri na kuwataka wananchi hususani wakulima
kukitumia vyema chakula walichonacho, hivyo aliwataka watendaji wa
halmashauri za wilaya, kata, vijiji, tarafa na wakuu wa wilaya za mkoa
huo kuanza kulisimamia kikamilifu agizo hilo.
Mkuu huyo wa mkoa aliwataka wananchi na wakulima katika wilaya za
mkoa huo kulima mazao yanayokomaa haraka kwa kutumia mvua kidogo
zinazonyesha, kuendeleza kilimo cha umwagiliaji maeneo yenye skimu za
umwagiliaji ili kuongeza kiwango cha uzalishaji wa nafaka za mazao ya
chakula.
Mkuu wa wilaya ya Kilosa, Adam Mgoyi, alisema hali ya chakula kwa
mwaka 2015/2016 halmashauri ilizalisha tani 123,128 za nafaka , wakati
mahitaji ya chakula cha nafaka kwa wilaya ni tani 103,957 na kwa takwimu
hizo wilaya bado inajitosheleza kwa chakula msimu wa 2015/2016.
Hata hivyo, alisema kuna baadhi ya maeneo yameanza kuonesha upungufu
wa chakula ambayo ni Magole, Kitete, Dumila, Maguha, Magumbike, Mamboya,
Mtumbatu, Mabula na Kidete.
Mkuu huyo wa wilaya alitaja sababu kubwa ni kukatika kwa mvua mapema kulikosababisha mazao hasa mahindi kutokomaa vizuri.
Hata hivyo, alitaja mikakati ya wilaya katika kutatua kero ya sekta
ya kilimo ni kuendelea kutoa elimu juu ya kukabiliana na mabadiliko ya
tabia nchi, kwa kuwafundisha wananchi kulima
CHANZO GAZETI LA HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment