Morogoro. Unaweza usiamini, lakini ndivyo ilivyokuwa Krismasi kwa mkazi wa Kitongoji cha Upangwaji, Kijiji cha Dodoma-Isanga wilayani Kilosa, Augustino Mtitu (42) kuchomwa mkuki mdomoni uliotokea shingoni.
Mtitu anayeaminika kuchomwa mkuki huo na wafugaji, amefanyiwa upasuaji uliochukua saa moja katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro na kufanikiwa kuutoa.
Pia, Mtitu ameshonwa nyuzi sita katika ulimi kutokana na jeraha kubwa alilopata katika kiungo hicho.
Majeraha hayo yapo kwenye ufizi, ulimi na sehemu ya nyuma ya shingo na yamemfanya ashindwe kuzungumza.
Mganga wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Frank Jacob amesema walimpokea Mtitu juzi saa 10 jioni kutoka Hospitali ya Wilaya ya Kilosa akiwa na mkuki huo mdomoni.
Mganga msaidizi wa meno wa hospitali hiyo, Judith Mwidunda amesema baada ya kufanyiwa upasuaji wa kutoa mkuki mdomoni, wamemfanyia uchunguzi na kubaini kuwa pia ameumia mfupa wa taya la juu na ulimi kuchanika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amesema jeshi hilo linawashikilia watu watatu na linaendelea na msako wa watu wengine na mmiliki wa mifugo iliyoingia shambani amefahamika.
Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ameitaka Serikali iwabaini wote waliohusika katika vitendo hivyo na kuhakikisha wanachukuliwa hatua kali za kisheria.
CHANZO GAZETI LA MWANANCHI
CHANZO GAZETI LA MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment