Na. Hassan Mabuye (Kitengo cha Mawasiliano - Wizara ya Ardhi)
Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi anaendelea na Ziara
zake za utatuzi wa Migogoro ya Ardhi nchini, ambayo imejikita zaidi
katika kutatua migogoro ya ardhi ya Mikoa ya kanda ya Magharibi,
Kaskazini na ile ya Kanda ya Ziwa hapa nchini.
Mhe. Lukuvi kwa siku
ya jumatatu tarehe 19 Desemba 2016 atatua migogoro ya ardhi ya wilaya ya
Musoma mkoani Mara na siku ya jumanne tarehe 19 Desemba 2016 atatua
migogoro ya ardhi ya wilaya ya Bunda mkoani Mara.
Katika ziara hiyo
Waziri Lukuvi atakutana na wananchi wa Musoma mjini na wananchi wa Bunda
walio na kero za migogoro ya ardhi na kuzitatua pamoja na kutembelea
miradi inayosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika wilaya
ya Musoma.
Aidha, Mhe. Lukuvi
baada ya ziara hiyo anatarajiwa kuwasili mkoani Arusha ambapo pia atatua
migogoro ya ardhi inayoukabili mkoa huo.
Hadi sasa Mhe. Lukuvi
ndani ya mwezi huu wa Desesmba ameishatatua migogoro ya ardhi ya Mkoa wa
Kigoma na wilaya zake za Kigoma mjini, Kasulu na Kibondo na katika Mkoa
wa Shinyanga na wilaya zake za Kishapu na Shinyanga mjini na katika
mkoa wa Geita amefanya ziara katika wilayani Chato.
0 comments:
Post a Comment