Na Ally Daud-MAELEZO
MOROGORO
WATUMISHI
wa Umma wametakiwa kufanya mazoezi ya viungo Mara moja kwa wiki ili
kujiepusha na magonjwa yasioambukiza ili kujenga watumishi wenye afya
imara kwa maendeleo ya taifa.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa magonjwa yasioambukiza (NCD) Prof.
Ayoub Magimba wakati Wa kufunga mkutano Wa siku tatu Wa Madaktari na
wadau Wa afya ngazi ya mkoa na wilaya katika kupata mpango mkakati wa
kujikinga na magonjwa yasioambukiza uliofanyika mkoani Morogoro.
"Katika mkutano huu wa kupata mpango mkakati wa kujikinga na magonjwa yasioambukiza tumeazimia kua na Sera inayoelekeza watumishi wote wa Umma wafanye mazoezi ya viungo siku moja kwa wiki ikiwa ni sehemu ya majukumu yao" alisema Prof. Magimba
Aidha
Prof. Magimba amesema kuwa mazoezi hayo ni sehemu ya majukumu ya
watumishi wa Umma ili kuwasaidia wale wanaokosa muda wa kufanya mazoezi
majumbani kwao ili kujikinga na magonjwa hayo.
Mbali
na hayo Prof. Magimba amesema kuwa watanzania wanatakiwa kuepuka
matumizi ya Mara kwa mara ya Sigara na vileo kwa pamoja na badala yake
wajikite kwenye mazoezi na utumiaji wa vyakula asilia.
Kwa upande wake Daktari bingwa Wa magonjwa ya ndani Dkt. Meshack Shimwela ambaye ni mshiriki wa mkutano huo amesema kuwa watanzania wanatakiwa kuzingatia na utekelezaji wa Sheria za barabarani ili kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na ajali mpaka kufikia mwaka 2030.
"Watanzania
hasa madereva wa vyombo vya moto wanatakiwa kuzingatia na kutii Sheria
za barabarani hususani kuacha kuendesha vyombo vyao wakati wamelewa ili
kupunguza asilimia 50 ya vifo vitokanavyo na ajali za barabarani hadi
kufikia 2030" alisema Dkt. Shimwela
Aidha
Dkt. Shimwela amesema kuwa katika mkutano huo wameadhimia kuishauri
serikali kutenga maeneo maalum ya kuvutia Sigara pamoja na kuweka muda maalumu wa kunywa pombe ili kujikinga na kuepuka magonjwa hayo.
Mkutano
huo uliokutanisha madaktari wa ngazi za mkoa na wilaya zote nchini
umelenga kutengeneza Sera na mikakati ya mwaka 2017 hadi 2020 katika kupambana
na magonjwa yasioambukiza kama kisukari, kansa,shinikizo la damu, ajali
za barabarani na uzito kuzidi kiasi ili kujenga taifa lenye afya na
Maendeleo.
0 comments:
Post a Comment