Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Badala yake, waisaidie serikali kutimiza malengo yake ya kukusanya
kodi ipasavyo na kudhibiti matumizi yasiyo na tija kuharakisha maendeleo
ya nchi.
Aidha akizungumzia bajeti ya wizara inayotarajiwa kuwasilishwa
bungeni wiki hii, Waziri Mpango alisema matumizi ya kawaida yamepunguzwa
na fedha nyingi zimeelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.
Dk Mpango alisema hayo hivi karibuni mjini Morogoro, wakati akizindua baraza jipya la wafanyakazi wa wizara hiyo mjini Morogoro.
Alisema jukumu kubwa la wizara hiyo ni kukusanya mapato na
kuyasimamia. Aliomba ushirikiano kutoka kwa wafanyakazi wote wa wizara
hiyo, watimize wajibu wao kufikia malengo hayo.
Aliwataka wataalamu hao kuhakikisha kuwa sera zinazotungwa zinakuwa
rafiki na hazibadiliki mara kwa mara ili kuvutia uwekezaji na wawekezaji
nchini.
Chanzo Gazeti La Habari Leo
0 comments:
Post a Comment