Home » » BILIONI 70.8/- ZAREJESHWA KUTOKA MIKOPO YA WANAFUNZI 138,803.

BILIONI 70.8/- ZAREJESHWA KUTOKA MIKOPO YA WANAFUNZI 138,803.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa.

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, imesema jumla ya Shilingi bilioni 70.8 zimerejeshwa kutoka kwa wanafunzi 136,803 kati ya 177,017 ambao walinufaika na mikopo hiyo.
 
Aidha, wengine  40,819 hawajaanza kurejesha mikopo Bunge limeambiwa, kadhalika Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB)  imeanza kuwachukulia hatua mbalimbali ili waanze kurejesha mikopo  hiyo mara moja .
 
Maelezo  hayo  yalitolewa jana bungeni na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa,  alipokuwa akijibi swali la Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige (CCM).
 
Mbunge huyo alitaka kufahamu  ni wanafunzi wangapi wamenufaika na mfumo wa mikopo ya elimu ya juu.
 
Pia, alihoji ni marejesho kiasi gani yamerejeshwa na wale wasiorejesha wanachukuliwa hatua gani kwa kutotejesha mikopo hiyo.
 
Akijibu swali hilo, Kawambwa alisema hatua zinazochukuliwa kwa wasiorejesha mikopo ni pamoja na majina yao kutangazwa kwenye vyombo vya habari vikiwamo Magazeti na Tovuti ya Bodi.
 
Pia, alisema baadhi ya wanufaika wameanza kushtakiwa Mahakamani kwa mujibu wa sheria.
 
Kuhusu hatua zilizochukuliwa dhidi ya wasiolipa mikopo kuwa Bodi iliwafunguliwa kesi wadaiwa 18 waliolipa mikopo yao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
 
Alisema kati ya hao, wadaiwa watano waliamuliwa kulipa madeni yao pamoja na faini wakati wengine 13 kesi zao zinaendelea kusikilizwa katika Mahakama hiyo.
 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa