Home » » UKAWA SASA KUTEGUA KITENDAWILI CHA MAJIMBO

UKAWA SASA KUTEGUA KITENDAWILI CHA MAJIMBO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399http://www.habarileo.co.tz/images/Ukawa.jpg
. KITENDAWILI cha mgawanyo wa majimbo ya uchaguzi kulingana na makubaliano ya Ukawa, kinatarajiwa kutenguliwa wiki hii viongozi wa vyama vinavyounda umoja huo vitakapokutana kukamilisha utaratibu wa kuachiana.
Hata hivyo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Dk Willibrod Slaa, kimesema vigezo mbalimbali vitaangaliwa ikiwa ni pamoja na sifa za mgombea, uwezo wake binafsi na kukubalika kwake na wananchi wa maeneo husika.
Dk Slaa alisema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika juzi kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege, Manispaa ya Morogoro.
Ingawa haikuelezwa maeneo yenye utata juu ya mgawanyo wa majimbo baina ya washirika wa Ukawa, wafuasi wa Chadema walimpokea Dk Slaa kwa mabango ambayo pamoja na masuala mengine, yalikuwa na ujumbe ulioonesha wanataka kufahamu hatma ya kuachiana majimbo, likiwemo la Morogoro Mjini.
Akihutubia, Dk Slaa ambaye alihimiza wapenzi wa chama hicho kuachana na siasa za shari, visasi, alisema wiki hii viongozi watakutana kukamilisha namna ya kuachiana majimbo ya uchaguzi.
“Hatujakaa kimya katika jambo hili ...wiki iyajo (wiki hii) tunakutana viongozi kukamilisha mapendekeo ya mgawanyo wa majimbo,” alisema na kusisitiza kwamba vigezo mbalimbalivitaangaliwa.
Profesa Lipumba Wakati Dk Slaa akihakikishia wafuasi wa chama chake juu ya hatma hiyo ya majimbo kujulikana wiki hii, pia Mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba, hivi karibuni akizungumza na gazeti hili, alisema suala hilo limepangwa kumalizwa Aprili 28, mwaka huu jijini Dar es Salaam, ambako viongozi vinavyounda umoja huo vitatu watakutana.
Vyama vingine vinavyounda umoja huo ni NCCRMageuzi chini ya James Mbatia na NLD ambacho Mwenyekiti wake ni Dk Emmanuel Makaidi.
Kulingana na maelezo ya Profesa Lipumba, viongozi kutoka vyama hivyo, watakaohusika katika majadiliano ya kina ni pamoja na wenyeviti wa vyama, makamu wenyeviti, makatibu na wajumbe wa sekretarieti kutoka ndani ya vyama hivyo watakuja kufikia makubaliano ya mwisho.
Baada ya kikao hicho ambacho vyama husika vitafikia mwafaka wa pamoja, ndipo itawekwa wazi juu ya majimbo husika likiwemo la Morogoro Mjini ambalo haijafikiwa maafikiano.
Ukawa ulianzishwa Februari mwaka jana wakati wa Bunge Maalumu la Katiba baada ya kushikamana katika kupinga Bunge hilo la kihistoria na baadaye kususa, kabla ya kusaini makubaliano kwa ajili ya kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi zote kuanzia udiwani, ubunge na urais.
Siasa za kiungwana Dk Slaa alitaka wanachama na wapenzi wa Chadema kuachana na siasa za na visasi badala yake, wafanye siasa za kiungwana.
Chanzo:Habari Leo

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa