. Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (Rahaco), imesema kiasi
cha Sh1.5 trilioni kinahitajika kukarabati reli ya kati ili iweze kurudi
katika hali yake ya kawaida.
Hayo yalisemwa juzi na mhandisi mwandamizi wa
miradi wa Rahaco, Maizo Mgedzi alipokuwa akitoa taarifa yake kwa Kamati
ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC). Kamati hiyo ilikuwa wilayani
Kilosa kukagua reli ya kati ambayo mara nyingi katika kipindi cha mvua,
imekuwa ikiharibikla kutokana na mafuriko.
Mgedzi alisema kama Shirika la Reli litatengewa
Sh500 bilioni kila mwaka, litaweza kuimarisha reli hiyo na hivyo kutoa
huduma bila kusuasua.
Alisema bajeti ndogo imekuwa kikwazo katika jitihada zake za kuboresha reli na huduma nyingine inazopaswa kuzitoa.
Mhandisi huyo alitoa mfano wa mwaka wa fedha ulioisha kwamba shirika hilo liliomba Sh174 bilioni, likapewa Sh29 bilioni.
Kwa upande wake, mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya
Hesabu za Serikali, Zitto Kabwe alisema ataiomba Serikali katika bajeti
ya 2015/2016, itenge fedha zaidi kwa shirika hilo.
Chanzo:Mwananchi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment