Meneja wa Mbuga ya wanyama ya Selous, Benson Kibonde akimpatia maelezo
kuhusu masalia ya injini ya mvuke iliyoachwa na Wajerumani, kwa Waziri
wa Maliasili na Utalii Lazao Nyalandu (kushoto), waziri huyo alipofika
katika mbuga hiyo, kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kupokea vifaa vya
kukabiliana na ujangili vilivyotolewa na serikali za Marekani na
Ujerumani kwa ajili ya Mbuga ya Selous leo
Waziri Nyalandu akitembela maeneo mbalimbali ya mbuga hiyo ya Selous
kabla ya kukabidhiwa vifaa hivyo ya kukabiliana na ujangili katika mbuga
ya wanyama ya Selous leo. anayemuongoza na Meneja wa mbuga hiyo

Mkurugenzi wa theNkoromo Blog, Bashir Nkoromo, ambaye alialikwa kwenye
hafla hiyo, akitazama mto Ruaha unaopita katika mbuga ya Selous
Waandishi wa habari wakiwa kwenye hafla hiyo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza maneno ya
Utangulizi kabla ya kukabidhiwa vifaa vya kukabiliana na ujangili kutoka
na serikali za Marekani na Ujerumani katika hafla hiyo. Kulia ni Balozi
wa Mrekani Mark Childress na waili kulia ni Balozi wa Ujerumani Egon
Kochanke
Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress akizungumza kabla ya kutiliana
saini na Nyalandu mkataba ya kukabidhiana vifaa hivyo. Kushoto ni
Balozi wa Ujerumani Egon Kochanke
Balozi wa Marekani Mark Childress na Waziri wa Maliasili na Utalii wa
Tanzania, Lazaro Nyalandu wakitiliana saini mkataba wa Marekani kuipa
Tanzania msaada wa mafunzo yakiwemo ya kikomandoo kwa askari wa
wanyamapori na vifaa vya kisasa vya kukabiliana na ujangili katika mbuga
ya wanyamapori ya Selous leo.
Waziri Nyalandu akibadilishana hati na Balozi wa Marekani, Mark
Childress baada ya kusaini mkataba huo. Kushoto ni Balozi wa Ujerumani
Egon Kochanke
Waziri Nyalandu akibalidilishana hati na Balozi wa Ujerumani Tanzania
Egon Kochanke, baada ya kutiliana saini mkataba wa ujerumani kuipa
Tanzania msaada wa vifaa vya kisasa vya kukabiliana na majangili katika
mbuga ya wanyama ya Selous leo
Waziri Nyalandu akimshukuru balozi huyo wa Ujerumani baada ya
kubadilishana hati walizosaini. kulia ni Balozi wa Marekani Tanzania
Mark Childress
Waziri Nyalandu akitoa maelezo baada ya kutiliana saini na mabalozi wa Marekani na Ujerumani
Vifaa mbalimbali vya kisasa vilivyotolewa na serikali za Marekani na
Ujerumani kwa ajili ya kukabiliana na majangili katika mbuga ya
wanyamapori ya Selous
Askari wa Wanyamapori Anita Albert akijaribu kionambali ambacho ni
miongoni vya vifaa vilivyotolewa kwa Tanzania na Seriali za Marekani na
Ujerumani kwa ajili ya kukabiliana na ujangili
Askari wa wanyamapori wakikagua mahema ambayo ni miongoni mwa vifaa vya
kisasa vilivyotolewa na serikali za Marekani na Ujerumani kwa ajili ya
kukabiliana na ujangili katika mbuga ya wanyamapori ya Selous. Picha
zote na Bashir Nkoromo wa
theNkoromo Blog
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment