“Baada ya utafiti wetu maeneo mbalimbali, tuliwaita
wafanyabiashara hasa wenye nyumba za wageni na kumbi za starehe,
tukawaeleza hali halisi ya maambukizi mapya ya Ukimwi na kasi ya
wagonjwa wapya, lakini hali ikawa ni ileile na wenye dhamana ya
kuwafutia leseni wafabiashara wa kumbi za sterehe wamekaa kimya licha ya
kuwasilisha ripoti yetu. Pia, ni kweli kwamba kumbi hizo zinachangia
kufuga machagundoa,” anasema Mbiaji.
Anasema kuwa mbali na kumbi za sterehe kuficha
kundi hilo kwa nyakati zote za mchana na usiku, lakini makahaba,
machangudoa na mashoga kwa nyakati tofauti wamekuwa wakiitaka Serikali
iwatambue.
“Kwanza machangudoa na mashoga wanataka Serikali
itunge sheria za kuwatambua ili wasinyanyapaliwe jamii wa tabia zao,
hata madaktari wanapohitaji matibabu kwa kuumizwa wakati wa ngono,
kuingiliwa kinyume cha maumbile au kupata maambukizi ya Ukimwi,” alisema
naibu meya huyo mstaafu.
Licha ya kutaka Serikali itunge sheria za
kuwatambua pamoja na shughuli zao, wanaitaka pia inunue (vilainishi),
mafuta maalumu na kondomu maalumu kwa kazi hiyo, ili wavitumie kwa lengo
la kuepuka kuumia wakati wa kutoa huduma kwa wateja wao.
Mbiaji anafichua siri za mashoga na machangudoa
akisema kwamba siku za Jumamosi, Jumapili na sikukuu zimekuwa za shida
kwao kutokana na kukosa wateja wa uhakika kutokana na wateja wao ambao
ni wanaume wa watu kutokwenda kazini kukosa mapato ya kutosha.
Manispaa kudhibiti
Kwa upande mwingine Manispaa ya Morogoro ilifanya
jitihada kuyatambua makundi ya machangudoa na mashoga, kisha kuyashauri
kuachana na kazi hiyo ikiwaeleza kuwa ipo tayari kuwapa mikopo ya riba
nafuu ili wafanye biashara halali.
Siyo hivyo tu, bali manispaa hiyo pia iliwaomba
wamiliki wa kumbi za sterehe kusaidia kushawishi makundi hayo kuachana
na kazi hiyo na kujiingiza katika biashara halali za ujasiriamali, jambo
ambalo hata hivyo halikufanikiwa.
“Wazazi nao wanapaswa kuwa makini na malezi ya
watoto wa jinsi zote hasa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwa
kuwadhibiti ili wasizurure ovyo na kutumia mwanya huo kuiga tabia chafu
za uchangudoa, ushoga na matumizi ya dawa za kulevya,” anasema Mbiaji.
Anaongeza: “Kinachoumiza zaidi ni wanafunzi wa
shule za msingi kujiingiza katika biashara hiyo. Tayari nao wameingia
rasmi kwenye biashara ya ngono kutokana na dada zao wa sekondari
kujiingiza.”
Mbiaji anasema kuwa manispaa iliunda kamati
kufuatilia makundi yaliyovamia mjini humo na kutoa mapendekezo ya
kufutiwa leseni za biashara kwa kumbi za sterehe zilizokiuka taratibu na
sheria za nchi, lakini wenye mamlaka na suala hilo wamekaa kimya na
tatizo kuendelea kukua siku hadi siku.
“Kazi ya kuyatambua makundi hayo ilifanyika kwa
upelelezi wa hali ya juu na ilishirikisha viongozi wanne wa dini za
Kiislamu na Kikristo, madiwani watatu, watendaji watatu wa halmashauri
nami nikaongoza jahazi.
Chanzo;Mwananchi
“Watu waliotuona walishindwa kutofautisha kwani wanawake wote
tulivaa nguo fupi, tulivaa kihuni ili kulingana na uhalisia na mienendo
ya machangudoa. Katika msafara huo wanaume walijifananisha na tabia za
mashoga,” anasema Mbiaji.
Anafafanua zaidi akisema: “Mambo ya aibu
yalionekana katika vyumba vya makahaba. Tulishuhudia wanaume wanne na
wanawake wanne wakiwa chumba kimoja, vitanda viwili wakifanya yao
tuliingia humo kwa kulipia fedha mlangoni, Sh1,000.
Mwenyekiti
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mwanzomgumu, Kata
ya Mwembesongo, Manispaa ya Morogoro, Saidi Omari Kamba (66) anasema
kuwa biashara ya ukahaba ipo katika mtaa wake eneo la Msamvu Itigi na
kwamba sasa biashara hiyo inatimiza mwaka wa pili.
Kamba anasema kuwa taarifa za wanawake hao kufanya
biashara ya ngono zimefika katika ofisi yake kutoka kwa wazazi
waliolalamikia tabia za machangudoa hao kuwa ni kero hasa kwa sababu
wanaenda kinyume na maadili huku wakiwa jirani na makazi ya watu
yanayojumuisha watoto ambao ni rahisi kuiga tabia hizo.
“Baada ya kupata taarifa za uwepo wa makahaba,
nilifanya uchunguzi na kubaini ukweli. Kingine nilichoelezwa ni kwamba
kuna tetesi za wanawake hao kupangisha moja ya nyumba na kulala mchana,
lakini giza likiingia hujisogeza eneo la Msamvu Itigi na kuanza kuuza
miili yao kwa wanaume lengo likiwa kupata ujira wa fedha,” anasema
Kamba.
Anaeleza kuwa miaka ya nyuma kulikuwa na kundi
kama hilo, lakini lilikuwa limejisitiri katika nyumba maalumu na athari
zake zilikuwa ndogo tofauti na sasa, ambapo wanawake hao wamekuwa
wakiuza miili yao eneo la wazimida ambayo watoto wanakuwa hawajalala.
“Tumefanya vikao vingi na wazazi kuhusu namna ya
kuwaondoa wanawake hao, lakini Serikali ya Mtaa haina ubavu wa
kuwaondoa. Suala hili tumelifikisha katika ngazi za juu, lakini nao
wamekaa kimya na kero imebakia kupokea malalamiko kila kukicha kutoka
kwa wazazi,” anasema Kamba.
Mfanyabiashara wa kwanza
Leonard Mwofuga mfanyabiashara aliyejenga kibanda
cha biashara eneo la Msamvu mwaka 2000, anaeleza historia ya eneo la
Msamvu Stendi na jinsi machangudoa walivyovamia akisema kuwa Februari
mwaka 2000, alianza kuweka kibanda cha biashara eneo hilo baada ya
Serikali kuhamisha stendi kuu ya mabasi yaendapo mikoani kutoka katikati
ya mji kwenda Msamvu, ambao sasa panajulikana kama Msamvu Itigi.
Kabla ya stendi kuhamishiwa Msamvu, eneo hilo
lilivuma kwa majina ya tofauti likiwamo Msamvu kwa Mela, Msamvu kwa
Lupilo, Msamvu Highway, Msamvu BP, lakini majina hayo yalipungua nguvu
tangu mwaka 2012, baada ya mfanyabiashara mmoja wa vinywaji kuhamia eneo
hilo na kundi la machangudoa na mashoga kutoka katikati ya mji.
Mwofuga anasema: “Eneo hili lina karaha ya kila
aina, hasa jua linapozama kwani utashuhudia utitiri wa machangudoa na
mashoga wakianza kutanda kando ya malori na nguo zao za nusu utupu,
wakiwasubiri wanaume kuwachukua na kwenda kufanya nao ngono.
Anasema kuwa kutokana na hali hiyo, eneo hilo huzagaa ovyo
mipira ya kiume, huku wafanyabiashara wakikosa wateja wa kununua bidhaa
za wafanyabiashara maeneo hayo, hasa wale viongozi wa serikali na watu
wanaojiheshimu kwa kukwepa fedheha katika eneo hilo.
“Mwandishi kama utapata muda, wewe njoo eneo hili
la Itigi hapa Msamvu saa 4 usiku utaona mwenyewe kinachofanyika na
utakiri niliyokueleza kuwa yote yana ukweli. Hapo nyuma kuna vibanda
vinavyotumiwa na machangudoa wa bei ya chini na wale wenye machangudoa
wenye kiwango cha juu humpeleka mteja wao katika vyumba vya kulala
wageni katika eneo hilo hilo,” anasema Mwofuga.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa miezi
mitatu mfululizo umebaini wanaume wanaofika eneo hilo la Msamvu Itigi
hutozwa viwango tofauti vya fedha kwa huduma ya ngono kulingana na aina
ya changudoa ambao wamegawanyika katika makundi mawili.
Makundi hao ni yale yanayotoa huduma ya ngono ya
kuanzia Sh2,000 hadi Sh4,000 na mteja akilazimika kuingizwa katika
kibanda ili akidhi haja zake katika godoro lililotandikwa chini ya
ardhi, huku mmiliki wa kipanda hicho akimtoza changudoa Sh1,000 kwa kila
mteja atayeingia naye kwenye vibanda vilivyopo nyuma vya
wafanyabiashara wa chakula na vinywaji.
Kundi la pili ni la machangudoa wa hadhi ya juu
ambao hutoza Sh5,000 na zaidi kisha kumpeleka mteja katika vyumba vya
kulala wageni iliyopo eneo hilo.
Hata hivyo, hatari wanayoweza kukumbana nayo
wateja wa machangudoa na makahaba hao ni iwapo watagundulika kuwa na
pesa na vitu vya thamani kwani anaweza kudhuriwa kwa kuwekewa dawa za
kulevya wakitumia mbinu za kiulaghai ikiwamo kulazimisha kunyonywa
matiti yake kabla ya kufanya ngono.
Masheikh wazungumza
Mjumbe wa Baraza la Masheikh Mkoa wa Morogoro,
Sheikh Ally Omari Ngarawa anaeleza kuwa kwa nafasi yake ya uongozi wa
dini ya Kiislamu alisikia taarifa hizo baada ya kuhudhuria mchezo wa
dhumna uliochezwa eneo la Soko Kuu la Mkoa wa Morogoro.
Ngarawa anasema kuwa ni jambo la aibu kwa viongozi
kufumbia macho na kuwaacha makahaba wakiendelea kufanya biashara ya
ngono kwa zaidi ya miaka miwili sasa katika manispaa hiyo.
“Siku moja nilisikia wanamichezo wa mchezo wa
dhumna wakiongea juu ya biashara ya ngono Itigi, lakini nilishtuka na
kutega sikio kusikia maneno hayo na sikuweza kuchangia mada hiyo bali
nilichofanya ni utafiti kwa wiki mbili na nilibaini ukweli huo,” anasema
Ngarawa.
Anaongeza: “Ni kweli ngono inafanyika, tena bila
kificho. Mwanamume akifika eneo hilo huchagua mwanamke anayependezwa
naye na kupatana bei ambayo ni kati ya Sh3,000 hadi Sh5,000. Wakati
mwingine hufikia Sh10,000 hii hutokana na matakwa ya mteja husika.”
Kwa mujibu wa sheikh huyo ambaye ni mwakilishi wa
Sheikh wa Mkoa wa Morogoro, lengo la kufanya utafiti huo lilikuwa
kufikisha ujumbe kwa waumini wa Dini ya Kiislamu nyakati za ibada, hasa
Ijumaa ambapo hufika msikitini kwa wingi na kutoa mahubiri mara nne kwa
mwezi moja
Polisi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro (RPC), Leonard
Paulo anasema: “Unataka kufahamu juhudi za Jeshi la Polisi katika
kuinusuru jamii na maporomoko ya maadili kwa jamii zinazozungukwa na
kumbi za starehe, nalifanyia kazi nami nijiridhishe ili nikupe taarifa
sahihi kwa lengo la kuelimisha jamii.”
Rais Kikwete
Akihutubia wananchi wa Mkoa wa Morogoro katika
Uwanja wa Jamhuri mapema mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete alieleza kuwa
ugonjwa wa Ukimwi unatafutwa na siyo ugonjwa wa bahati mbaya.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment