Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAKULIMA wa mboga mboga na viungo wilayani Kilosa mkoani hapa, wameiomba serikali, taasisi, kampuni na watu binafsi nchini kote kujitokeza kuwekeza katika kuongeza thamani, ufungaji bora na kuwezesha mazao hayo kudumu muda mrefu ili wanufaike nayo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye ziara ya mafunzo
iliyoandaliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa na mashirika ya kiraia ikiwemo Mviwata, Ibrahim Mlima na Nasibu Hussein, waliomba viwanda hivyo ili wanufaike na kilimo hicho, ambacho kwa sasa kimefikia zaidi ya asilimia 50 ya wanachozalisha kuharibikia shamba.
Walisema ziara hiyo iliyowakutanisha wakulima wa vijiji vya Kibunga, Ulaya na Mbuyuni katika bustani za Kijiji cha Ibingu, imewafumbua macho baada ya kubaini kuwa
mazao mengi ya wazalishaji nchini yanaharibikia shamba kwa kukosa viwanda kama hivyo.
Awali, Ofisa Kilimo kutoka Mviwata, Amanzi Amanzi, aliwataka wasomi nchini kuanza kubuni njia zitakazofanikisha kutegua changamoto ya upotevu wa
mazao mashambani, ili yawanufaishe wakulima ambao wengi wao huishia kubaki na madeni baada ya kuzalisha.
Aidha, aliwataka maofisa ugani kutekeleza kwa vitendo kazi na fani waliyosomea, kwa kuwa karibu na wakulima hususani kipindi hiki cha kuelekea utayarishaji wa mashamba hadi kuvuna ili wazalishe kwa tija.
CHANZO:TANZANIA DAIMA
0 comments:
Post a Comment