Home » » NHC YATOA MAFUNZO UFYATUAJI TOFALI ZA KISASA

NHC YATOA MAFUNZO UFYATUAJI TOFALI ZA KISASA

VIJANA 40 wilayani hapa, wameanza mafunzo ya siku saba kufyatua tofali za kisasa ili kusaidia kupunguza uharibifu wa mazingira pia kuondosha tatizo la ajira na kuinua kipato kwa vijana.
Mratibu na msimamizi wa mafunzo hayo yanayotolewa na Shirika la Nyumba Nchini (NHC), Castol Malulika, alisema lengo la mpango huo ni kuharakisha maendeleo kwa kuboresha ujenzi wa makazi bora kwa gharama nafuu.
Malulika alisema NHC imetoa mashine nne kwa vijana na mafunzo hayo pamoja na sh. 500,000 zinazotarajiwa kutolewa kwa kila kikundi kitakachoanzishwa kwa kazi hiyo kama ruzuku ya mtaji.
Baadhi ya vikundi vilivyoanza kunufaika na mafunzo hayo kwa mujibu wa mratibu huyo ni pamoja na Mtandao Mbasa toka Kata ya Kibaoni, Ujenzi Lumemo toka kata ya Lumemo,Vijana Mlabani na Vijana Wandewa vyote kutoka kata ya Ifakara.
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Hassan Masala, ameishukuru NHC kwa kubuni mpango huo kwani utaongeza ajira kwa vijana na ujenzi wa nyumba bora zenye gharama nafuu na wao kama wilaya watazidi kuwahimiza na kuwahamasisha vijana wengi kuingia katika shughuli hii.
Pia amewaagiza vijana kuwa elimu watakayoipata ni vyema kuitumia ipasavyo katika ujenzi wa nyumba bora na zenye gharama nafuu.
Chanzo:Tanzania Daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa