Home » » AGIZO LA JK KILOSA LAIBUA MAPYA

AGIZO LA JK KILOSA LAIBUA MAPYA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
KAULI ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa hivi karibuni kwa uongozi wa Wilaya ya Kilosa mkoani hapa kuhakikisha wamepima viwanja ndani ya wiki moja kuwagawia wahanga wa mafuriko na kuwasaidia ujenzi, limepuuzwa na kusababisha wahanga hao kukusudia kuonana naye.
Hata hivyo, uongozi wa Halmashauri akiwemo Mkurugenzi, Idd Mshili na Mwenyekiti, Ameir Mubarak, wamekanusha wakibainisha kuwa kuchelewa kwa zoezi hilo kunatokana na mgongano wa idadi ya majina ya waathirika, ambako halmashauri kuna
waathirika 500 na uongozi kambini 576. 
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro, Mwenyekiti wa wahanga hao kambi ya Mansulia, Mathew Gervas, alisema mbali
na kumpuuza rais katika agizo lake, viongozi wanamdhihaki wakisema hana ardhi ya kugawa bure wilayani
humo.
“Upuuziaji huu hakuanza leo, kwanza baada ya mafuriko mwaka 2010 alituahidi viwanja na ujenzi wa makazi ya kisasa kwa wote tuliokumbwa na mafuriko…alipokuja mwezi jana akashangazwa na kutotekelezwa agizo lake na kutoa wiki moja kwa halmashauri mbele ya mkurugenzi kutekeleza,” alifafanua na kuongeza.
Rais mbele ya wananchi aliagiza bila upendeleo, viwanja hivyo wapewe watu wote walio kambini na serikali ianze kusaidia ujenzi ili wancahi hao waondokane na adha ya kambi za mabati na asingependa kuondoka madarakani wahanga hao
wakiwa makambini.
Alisema, walipoona hakuna dalili yoyote ya utekelezwaji agizo hilo, Agosti 29 na Septemba Mosi uongozi wa wahanga kambi ya Magomeni ulikutana kwa nyakati tofauti na
uongozi wa halmashauri lakini uliwashangaza kwa mkanganyiko
wa kauli zao.
Alifafanua kuwa, Mwenyekiti wa Halmashauri alidai Kilosa hakuna ardhi ya Rais, akiwataka waende Ikulu wakati Mkurugenzi aliukana uongozi wa wahanga kambini, wasitegemee viwanja vya bure na kuwa hautambui uongozi na taarifa za kambini, badala yake anafanya
kazi na viongozi wa vitongoji.
“Binafsi nikwambie kuwa hao wanataka kutuchonganisha tu na
kiongozi wetu! Tunaheshimu kauli yake ila wanataka kutumia
agizo hilo kunufaisha watu wengine, sasa sisi halmashauri tumesema watakaogawiwa maeneo ni waliyokuwa wamiliki wa nyumba tu na orodha tunayo,” alifafanua Mwenyekiti Ameir.
Chanzo; Tanzania Daima 

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa