Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
BAADA ya juhudi za wakulima 300 wa Mgulu wa ndege Manispaa Morogoro
kushindwa kupenyeza hoja ya dhuruma ya ardhi kwa Rais Jakaya Kikwete
mwishoni mwa wiki, wanakusudia kumfuata kwenye ziara atakayofanya leo
mkoani hapa.
Wakizungumza na Tanzania Daima jana Zaolo Mkude na Betrice Zacharia
walisema uamuzi wa kuufuata msafara huo ni kuhakikisha madai yao
yanafika kwa rais baada ya kupuuzwa na mamlaka za chini.
“Sisi ni waathirika wa ardhi ile kisheria maana tuliishi hapo kwa
miaka 30 kabla manispaa haijaja kupima kwa mabavu na kutufukuza…
tutamfuata wilaya nyingine tukamkabidhi madai yetu,” alisema Betrice.
Walisema mgogoro huo wa muda mrefu unatokana na ubinafsi wa watendaji
wa manispaa kutowalipa fidia, kupuuza zuio la Mahakama, kuendelea
kugawa kwa nguvu maeneo yao, kutishia kuwafunga na kupigwa mabomu kwa
kisingizio cha kuhatarisha amani.
“Ukweli ziara hii tulitegemea kupata jibu la moja kwa moja kwa rais
Kikwete juu ya hatima ya maeneo yetu ya Mgulu wa ndege kama angetoa
nafsi kumweleza kero zetu.
“Tunaomba tueleweke kuwa hatupingani na maendeleo… shida hapa ni haki
yetu juu ya ardhi tunayotakiwa kuiachia,” alifafanua Mkude.
Akihitimisha kwa awamu ya kwaza ziara yake mkoani Morogoro katika
uwanja wa Jamuhuri, rais Kikwete hakuridhishwa na utendaji wa serikali
mkoani hapa akisema umejaa uzembe na uoga katika kusimamia na kutekeleza
shughuli za maendeleo
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment