Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAZIRI wa Maendeleo ya
Jamii Jinsia na Watoto, Sophia Simba amewashauri vijana nchini kujikita
katika shughuli za kilimo ili waweze kujiajiri wenyewe na kuinua kipato
chao badala ya kukaa vijiweni.
Hayo alisemwa jana
wakati akikagu baadhi ya mabanda na vipando vilivyopo katika uwanja wa
maonesho ya kilimo ya Julius Kambarage Nyerere mjini Morogoro.
Simba alisema kuwa
wakati sasa umefika kwa vijana kuacha kukaa vijiweni ama kuilalamikia
serikali kuhusu kukosa ajira na badala yake wajiunge kwa pamoja katika
kufanya shughuli za kilimo na ufugaji, kwani kilimo ndio ajira mama hapa
nchini.
"Nawahimiza vijana wote
kuacha tabia ya kutopenda kujishughulisha na kubaki kulalama kuwa
serikali haijawapatia ajira, kwani wanayo fursa kubwa ya kujikwamua
kiuchumi, endapo watajikita kikamilifu kwenye kilimo.
Aidha aliwataka
washiriki wa maonesho ya wakulima kuhakikisha wanalima kilimo chenye
ubora wakisaidiwa kikamilifu na maofisa ugani katika kuwapatia mbinu
bora za kilimo.
Katika hatua nyingine,
aliwakemea baadhi ya maofisa ugani wasio waadilifu na wanaowatoza fedha
wakulima pindi wanapohitaji kuhudumiwa ama kupata ushauri wa kitaalamu
katika kilimo, kwani ni kinyume na sheria na maadili ya kazi.
"Nakemea vikali baadhi ya maofisa wa kilimo wanaodai fedha kwa wakulima ama wafugaji wetu ili kutoa huduma," alisema.
Kwa upande wake mjumbe
wa kamati ya uratibu Kanda ya Mashariki Yahya Kijoli aliishauri wizara
hiyo kuweka mpango maalumu wa kuwabadilisha vijana kimtazamo hasa suala
la ajira, kwani wengi wao wamekuwa hawajishughulishi.
"Tunaiomba serikali
ielekeze zaidi katika kuunda mfumo utakowabadilisha vijana kimtazamo ili
wapende kilimo kwani wamekuwa wakiona kilimo kuwa ni cha watu wasio
wasomi,"alisema.
Hata hivyo waziri
alisema ili vijana wabadilike mtizamo ni lazima mabadiliko hayo yaanzie
ngazi ya familia, kata, vijiji na hata vitongoji kwani serikali haiwezi
kujenga utaratibu kwa nchi nzima bali kupitia ngazi kuu ya serikali ni
kuweka mazingira mazuri kwa hayo ambayo vijana wanataka kutekelezwa
Chanzo:Majira
0 comments:
Post a Comment