Home » » WASANII MORO WAMLILIA JK

WASANII MORO WAMLILIA JK

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
WASANII mkoani Morogoro wamemsihi Rais Jakaya Kikwete awasaidie kupata kituo cha redio na televisheni itakayokuwa na kazi ya kuibua na kukuza vipaji kabla hajamaliza muda wake.
Ombi hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki mbele ya Mkuu wa Mkoa, Dk. Joel Bendera katika utoaji tuzo ya vipaji ‘Moro Town Talent Awards’ na uzinduzi wa jengo la kuandalia kazi za wasanii.
Wasanii hao, pia waliwasilisha ombi kwa uongozi wa mkoa, kwamba Morogoro iwe kitovu cha usanii nchini kutokana na historia yake katika tasnia hiyo.
Mbele ya mkuu huyo aliyewakilishwa na Ofisa Tarafa ya Manispaa, Pakala Pakala Mulenge, Mkurugenzi wa kituo hicho na mwenyekiti wa wasanii mkoani hapa, Mohamed Ngwenje, alisema kilio cha wasanii kupata vituo vya habari ni kuikuza haraka tasnia hiyo na kuepuka vikwazo vilivyopo.
“Tunaamini unao uwezo, tufikishie salamu hizi kwa rais na tuwezeshe kupata eneo litakalobeba aina zote za sanaa kama vyumba vya masomo, kumbi za mazoezi, kurekodi na vituo vya habari… itakuwa ya kwanza Afrika na duniani kuanzishwa na serikali na itasaidia kutoa ajira kwa vijana ndani na nje ya nchi,” alisema Ngwenje.
Akijibu ombi hilo kwa niaba ya mkuu wa mkoa, Pakala Pakala alisema wazo la wasanii hao ni zuri kwani linalenga kukabili bomu la ajira kwa vijana na serikali kwa kadiri ya uwezo wake itajitahidi kulitafutia ufumbuzi.
Katika uzinduzi huo, waandishi wa habari, vyombo vya habari, wasanii katika fani mbalimbali, watu binafsi, taasisi, mashirika na makampuni walitunukiwa tuzo ya umahiri na Moro Talent Award
Chanzo;Tanzania Daima 

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa