Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KITUO cha kuibua na kukuza vipaji vya wasanii mkoani hapa, Moro
Talent, kimewatunuku tuzo maalumu za umahiri wa habari za kijamii 2014
waandishi mbalimbali akiwamo Joseph Malembeka wa gazeti hili.
Sambamba na Malembeka kupokea tuzo hiyo iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa
wa Morogoro, Joel Bendera, mwishoni mwa wiki, pia viongozi wa umma na
binafsi katika ngazi mbalimbali, wafanyabiashara, wasanii na wadau
mbalimbali walitunukiwa.
Wengine waliotunukiwa ni Mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa Habari
Mkoa wa Morogoro (MOROPC), Idda Mushi, Mratibu MOROPC Thadei Hafigwa,
John Nditi na Prince Baina Kamukulu.
Kabla ya kutolewa tuzo hizo, Mratibu wa Moro Talent Award, Mohamed
Ngwenje, alisema uamuzi huo umetokana na agizo la mkuu wa mkoa huyo
mwaka jana, kukitaka kituo hicho kutambua kazi za wasanii na
kuzitangaza kwa nguvu zaidi.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment