Home » » TUKIO KATIKA PICHA: MADEREVA WAKERWA NA TABIA YA ASKARI WA USALAMA WA BARABARANI KWA TABIA YAO YA KUJIFICHA PORINI NA TOCHI ZAO KISHA WAKIONA GARI LINAKUJA NDIO WANACHOROPOKA WAKIWA WAMELIPIMA KUTOKA HUKO HUKO PORINI.

TUKIO KATIKA PICHA: MADEREVA WAKERWA NA TABIA YA ASKARI WA USALAMA WA BARABARANI KWA TABIA YAO YA KUJIFICHA PORINI NA TOCHI ZAO KISHA WAKIONA GARI LINAKUJA NDIO WANACHOROPOKA WAKIWA WAMELIPIMA KUTOKA HUKO HUKO PORINI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Kwanza tuanze na swali la msingi kabisa hivi ni sawa kabisa kwa Askari wa usalama wa barabarani kujificha porini na kupima mwendo kasi wakiwa huko huko maporini baada ya kukaa barabarani ambapo ni peupe na kwenye hivyo vibao vinavyo onesha mwendo kasi?

Imekuwa ni Tabia sasa ambapo Askari hao wa usalama wa Barabarani hasa wenye tochi kujificha katika vichaka kisha wakiona gari linakuja wanapimia huko huko na kuja kumwandikia muhusika cheti, Cha kushangaza zaidi utakuta wanapima mwendo kasi kabla hata ya hicho kibao kuonekana.

Jambo hili linaonekana ni hatari hata kwa usalama wao binafsi kutokana na kwamba muda mwengine inawezekana Dereva yupo kasi na asimuone na kuweza kumsababishia madhara 

Hizi ni Baadhi ya picha za vibao vya mwendo kasi vilivyopo vichakani.
 Kwa kukaa huku kichakani na Tochi je huo mwendo kasi unapimwaje?
 Kichakani sasa hapa unachoropoka Ghafla kuna kuwa na usalama kweli hapa




 Picha zote na Morogoro yetu
 

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa