Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
ZAITUNI Ally (30) mkazi wa manispaa ya Morogoro amepandishwa
kizimbani katika Mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Morogoro kwa tuhuma za
kujeruhi na kumdhalilisha mwanamke mwenzie kwa kumtembeza mtupu mbele
za watu.
Akisoma maelezo ya shitaka hilo, Mwendesha Mashtaka wa Polisi,
Aminata Mazengo alidai mbele ya Hakimu Nuruprudensia Nassari kwamba
mtuhumiwa huyo alitenda makosa mchana wa Julai 5 mwaka huu eneo la
Msamvu B.
Ilidaiwa kwamba bila halali na akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria,
mshtakiwa alimkata Rehema Juma na kitu chenye ncha kali sehemu
mbalimbali za mwili wake na kumsababishia maumivu.
Mwendesha mashataka huyo aliendelea kudai mahakamani hapo kwamba siku
hiyo hiyo mtuhumiwa alimdhalilisha majeruhi huyo kwa kumlazimisha
kutembea mtupu mbele za watu.
Hata hivyo, mtuhumiwa alikana makosa hayo na yupo nje kwa dhamana
hadi kesi hiyo itakapotajwa tena Julai 24 mwaka huu kwa kuwa upelelezi
haujakamilika.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment