Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Ujenzi,Dk. John Magufuli
Wananchi hao ambao ni Hemed Abdallah, Daud Msigwa, Jorum Bioswaro, Rabbo Thobias, Johar Solomon na Saleh Ally wameandika notisi hiyo kwa Katibu Mkuu Wizara hiyo wakitaka walipwe kiasi hicho cha fedha kupitia kwa wakili wao wa kampuni ya Infinity Law Attorney’s.
Afisa Habari wa Wizara hiyo, Segolena Francis, alipoulizwa alisema hana uhakika kama barua hiyo imeifikia wizara au la kwa sababu Katibu Mkuu wa wizara, Mussa Iyombe, amesafiri.
“Katibu Mkuu amesafiri hayupo, lakini kwa sababu hajasafiri na ofisi nitawasiliana na Naibu Katibu Mkuu kuhusu suala hili na nitakuwa majibu,” alisema Segolena.
NIPASHE imefanya jitihada za kumtafuta Katibu Mkuu wa wizara hiyo pamoja na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, bila mafanikio kutokana na maelezo kuwa wapo nje ya nchi.
Wakili wa wananchi hao katika notisi yake ya barua yenye kumbukumbu namba ILA/DN/KIBAMBA/2014/1, anasema wananchi hao walibomolewa nyumba zao na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) bila kuzingatia sheria na kusababisha wapate hasara kubwa kutokana na nyumba zao kuvunjwa.
Wakili Mandele alisema kutokana na hali hiyo, Wizara hiyo inapaswa kuwalipa wananchi hao fidia ya Sh. milioni 444 kutokana na kuvunjiwa nyumba zao kinyume cha sheria na pia ilipe Sh. milioni 200 waliokuwa wapangaji wa nyumba hizo ambao vifaa vyao viliharibiwa wakati wa zoezi la kubomoa.
“Tunaagiza Wizara kuwalipa wateja wetu kiasi hicho cha fedha ndani ya siku 90 na kama itashindwa kufanya hivyo, tutafungua kesi mahakamani kudai fidia na hasara iliyopatikana,” alisema Wakili Mandele katika barua yake ambayo pia nakala amepeleka kwa Mwanasheria Mkuu wa serikali.
Mmoja wa waathirika wa kuvunjiwa nyumba, Rabbo Thobias, alisema nyumba zao zilizobolewa hazikuwa ndani ya hifadhi ya barabara ambayo kisheria ni mita 30, lakini Tanroads waliamua kuzibomoa kwa makusudi.
“Nyumba zetu zilizobomolewa zipo umbali wa mita 123 kutoka katikati ya barabara ya Morogoro wakati sheria inasema eneo la barabara ni mita 22.86 ambayo imeongezwamwaka 2010 na kuwa mita 30,” alisema.
Walisema Waziri Magufuli hataki kutii sheria za nchi, hataki kutii maamuzi ya mahakama na kwamba anachofanya ni ubabe kwa kuwa suala hilo liliamuliwa na mahakama kwamba hawakujenga nyumba zao ndani ya hifadhi ya barabara.
SOURCE:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment