Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
TAASISI ya Tanzania Women Health Network (TWHN), imebaini kuwa
zaidi ya asilimia 62 ya watoto katika Manispaa ya Morogoro, wamefanyiwa
ukatili wa kisaikolojia, jinsia na kimwili na watu wa karibu, wakiwemo
ndugu na jamaa.
Hayo yamo kwenye taarifa fupi ya uzinduzi wa taasisi hiyo iliyosomwa
na Mkurugenzi wake, Gloria Kasilo kwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said
Amanzi, aliyewakilishwa na Ofisa Elimu Taaluma wa manispaa hiyo,
Christopher Wangwe.
“Ukatili mkubwa uliobainika katika utafiti huu hususani shule moja ya
msingi iliyotumika kama sampo ni ngono, kutumika kutafuata riziki,
kupigwa, kutumikishwa majumbani na kutishwa na wengine kufichwa,”
alisema.
Alisema lengo la taasisi hiyo ni kumwezesha mwanamke hasa mtoto wa
kike kujikomboa kwa kupata elimu itakayomwezesha kuzikabili changamoto
katika mazingira walipo na hatimaye kujiletea maendeleo.
Wangwe mbali na kuahidi kuunga mkono taasisi hiyo ili kufikia mpango
wa serikali wa Matokeo Makubwa Sasa, aliziomba taasisi na asasi zote
za kiraia kusaidia kudhibiti vitendo hivyo pamoja na wimbi la matumizi
ya dawa za kulevya.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment