Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAKAZI wa Kijiji cha Lubungo A, Kata ya Mikese, wilayani Morogoro,
wamevamia shamba linalodaiwa kupewa mwekezaji kinyemela na uongozi wa
kijiji wakishirikiana na wilaya na kugawiana kisha kukesha wakifyeka
msitu.
Uvamizi huo unaohusisha eneo hilo linalokadiriwa kuwa na ukubwa wa
ekari 1,000 unatokana na wanakijiji hao kubaini kuwa eneo hilo ambalo
hawajawahi kulipangia matumizi linakodishwa kwa watu wengine.
Wakizungumza kwa nyakati toafuti, Shabani Salumu, Ester Daud na
Hussein Mzuri, walisema wamechoshwa na rushwa kwa viongozi wao na kuuza
eneo lote kwa wawekezaji bila kuwashirikisha.
“Hapa kijijini tunakadiriwa kuwa zaidi ya watu 2,400 na tumezaliana
hadi hatuna eneo la kutanulia kijiji kwa shughuli za maendeleo na
uzalishaji, leo eneo linauzwa kinyemela, sisi na vizazi vyetu twende
wapi?” alihoji Salumu.
Kwa upande wake, Ester alisema viongozi wamekuwa wabadhirifu wa ardhi.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Juma Mgunda mbali na kukiri kuwepo
ongezeko la wananchi kijijini hapo na eneo kupungua, alikanusha kuuza
eneo hilo huku akiutupia lawama uongozi uliopita.
“Eneo lenye mzozo kwa mujibu wa kumbukumbu zangu linaonyesha ni mali
ya padri ambaye naambiwa anaitwa Father Seti na alilipata mwaka 1996
akiwa na lengo la kujenga chuo, ili watoto wanaohitimu katika maeneo
yetu wapate ujuzi,” alisema Mgunda.
Alisema ingawa wananchi hao wamevamia, lakini hawakupaswa kufanya hivyo.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment