Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, amewaagiza wakurugenzi wa
wilaya mkoani hapa kupeleka haraka taarifa za watumishi wazembe na
wasio waadilifu ofisini kwake, ili awachukulie hatua za kisheria.
Bendera alitoa agizo hilo mjini hapa juzi katika kikao cha madiwani
wa Halmashauri ya Morogoro cha kupitia majibu ya hoja za Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (GAG) mwaka 2012/ 2013.
“Muda wa kuleana umepita, nileteeni majina ya watu wasiowajibika na
wasio na uadilifu niwashugulikie… ni aibu kuwa na lundo la watu eti
watumishi ofisini wakati ufanisi wake ni ziro,” alisisitiza Bendera.
Alitoa kauli hiyo baada ya kusoma taarifa ya CAG ambayo imeonyesha
mkoa huo kufanya vizuri katika hesabu zake, hususani katika Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa na mamlaka za serikali za mitaa na kupata hati safi kwa
mwaka 2012/2013.
Pamoja na mkoa kupata hati safi, Bendera aliwataka watumishi wake
kutoridhika na mafanikio hayo na badala yake waendelee kupambana, ili
kudumisha mafanikio kwa lengo la kufikia kiwango cha juu kabisa.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment