Home » » MWENGE WAZINDUA MIRADI SABA YA BIL.1/-

MWENGE WAZINDUA MIRADI SABA YA BIL.1/-

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mwenge wazindua miradi saba ya bil.1/- MIRADI saba yenye thamani ya sh 1,029,561,685 imezinduliwa na mbio za mwenge wa uhuru wilayani Kilombero, mwaka huu.
Akizungumzia hilo mjini hapa jana, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Hassan Masala, alisema kati ya miradi hiyo mmoja ni maabara ya Shule ya Sekondari Mlabani, Ifakara.
“Miradi miwili ukiwemo wa nyumba ya mganga Sagamaganga na mashine ya kusaga na kukoboa Mang’ula A, imezinduliwa na miradi mitatu ukiwemo wa barabara ya lami ya Uhuru Ifakara, mradi wa maji Signal na Ofisi ya Kijiji Mang’ula A imewekwa jiwe la msingi,” alifafanua Masala.
Kwa mujibu wa Masala, mwenge huo ulikagua na kujionea miradi ya vikundi vya wanawake, wanaume, vijana, mradi wa ufugaji nyuki na hifadhi ya mazingira na shughuli za kupambana na kuzuia rushwa.
“Kati ya fedha hizo, sh milioni 136.9 zimechangwa na wananchi, sh milioni 463.8 serikali kuu, sh milioni 5.8 halmashauri na wahisani sh milioni 422.9,” alisema.
 Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa