Home » » MAADHIMISHO YA SIKUKUU ZA MEI MOSI MOROGORO

MAADHIMISHO YA SIKUKUU ZA MEI MOSI MOROGORO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Picha na Juma Mtanda Blog
Daktari mtaalamu wa nusu kaputi katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro, Doward Lulambo kulia akiongoza mfano wa kumzalisha mama mjamzito kwa njia ya operesheni wakati wa maadhamisho ya kilele cha siku ya wafanyakazi duniani yaliyoadhimishwa katika uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro.

Mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amanzi (katikati) akiwa ameshikana mikono na Katibu Tawala Msaidizi Miundombinu mkoa wa Morogoro, Lucas Mwaijaka kulia na Bujaga Kagado ambaye ni Mwenyekiti wa Tucta mkoa wa Morogoro katika sherehe hizo.
Sehemu ya wafanyakazi.
 Meya wa Manispaa ya Morogoro Amir Juma Nondo (Mwenye koti) kushoto wakicheza kwaito.
Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Said Amanzi akihutubia wafanyakazi.

Hawa ndiyo wenye sherehe shirikisho la vyama vya wafanyakazi Morogoro (RAAWU) wakiongoza maandamano ya maadhimisho ya kilele cha Mei Mosi 2014 ambayo yalifanyika uwanja wa jamhuri Morogoro.







 Cakatapili likionyesha mbwembwe wakati likipita mbele ya mgeni rasmi

 Huyu ni mnyama swala aliyekaushwa aliyeletwa hifadhi ya taifa ya Mikumi

Gari la kampuni ya tanseed international Morogoro likiwa limebeba miche ya mahindi yenye mazao kupitia mbegu bora za tani 250 mbele ya mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amanzi (hayupo pichani ) wakati wa maadhamisho ya kilele cha siku ya wafanyakazi duniani yaliyoadhimishwa katika uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro.

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa