Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wafanyabiashara wakichambua vitunguu katika soko ya vitunguu la Misuna
mjini Singida baada ya msimu wa kuvuna na kuuza vitunguu kuanza. Gunia
moja linauzwa kwa bei ya sh120,000
Wajasiriamali katika Manispaa ya Morogoro, wameshauriwa kutumia
fursa zilizopo katika Mradi wa Uhusiano wa Maendeleo ya Kiuchumi (MPED),
ili kuboresha vipato vyao.
Mwezeshaji wa Mkusanyiko wa Wajasiriamali wa
Manispaa ya Morogoro, Martina Pangani, alisema mradi huo umeanzishwa kwa
ushirikiano wa manispaa na mji wa Kitchener, nchini Canada.
Alisema mradi huo ni wa manufaa kwa wajasiriamali
na kwa msingi huo kuna haja ya watu kujitokeza na kutumia fursa hizo
kikamilifu.
Hata hivyo, alieleza masikitiko yake kuhusu
wajasiriamali kucheleweshewa vibali vya kusambaza bidhaa zao ndani na
nje ya nchi, jambo linalowakatisha tamaa. Pangani aliliomba Shirika la
Viwango Tanzania (TBS), kujenga utamaduni wa kukagua bidhaa za
wajasiriamali hao na kutoa vibali kwa haraka.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Mkusanyiko
huo, Ibrahim Sanane, alisema mkusanyiko huo utawasaidia wajasiriamali
kubadilishana uzoefu kuhusu kutengeneza bidhaa bora.
Sanane alisema wajasiriamali wengi nchini
wanakabiliwa na tatizo la kukosa masoko, jambo linalowalazimisha
kuzalisha bidhaa kwa kiwango kidogo.
Wajasiriamali wanaounda mkusanyiko huo ni wa sekta za usagishaji wa nafaka, utalii, ufugaji kuku, mbao, nguo na nyama.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment