Home » » MKANDARASI ATEKELEZA UJENZI WA SOKO LA GEZAULOLE

MKANDARASI ATEKELEZA UJENZI WA SOKO LA GEZAULOLE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
MKANDARASI, Serico Company Ltd anadaiwa kutoweka na kutelekeza ujenzi wa Soko la Gezaulole, Kata ya Kauzani, Manispaa ya Morogoro linalotarajiwa kugharimu sh milioni 12 hadi kukamilika.
Hayo yamebainika kwenye ziara ya kukagua miradi ya maendeleo iliyoandaliwa na Kamati ya Fedha na Uongozi ya Baraza la Madiwani Manispaa ya Morogoro.
Akitoa ufafanuzi wa kushindwa kutekelezwa kwa baadhi ya miradi, Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, Hate Ngesya, alisema mradi huo umekuwa ukitelekezwa na makandarasi kila wakati.
“Mkandarasi wa kwanza Ommetech Contractors ambaye alikuwa amejenga hadi hatua ya upauji alikuwa ametumia sh milioni 29.7,” alisema Ngesya.
Alisema mradi huo ulibuniwa na wananchi mwaka 2005 kwa lengo la kusogeza huduma hiyo.
Alisema kiasi hicho cha fedha zilizokuwa zimetolewa kwa mkandarasi wa pili ni kwa ajili ya shughuli za kuingiza maji chooni, kutengeneza ngazi na kumalizia matungilizi katika ofisi za soko.
 Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa