Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MAKOVU ya kudumu kwa wanawake wengi nchini husababishwa na utoaji
mimba pamoja na utumiaji wa vidhibiti mimba ambayo ni hatari kwa afya
zao.
Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa juzi na Mkurugenzi wa Shirika la
Kutetea Uhai (Prolife), Emil Hagamu, kwenye mafunzo juu ya utumiaji wa
vidhibiti mimba kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Jodani na Chuo cha
Uandishi wa Habari cha Morogoro (MSJ).
Hagamu alisema vidhibiti vina madhara makubwa kwa watumiaji ambavyo vinaweza kuhatarisha maisha na kusababisha kifo.
“Kuna madhara mengi yakiwemo kuharibika ubongo, moyo kwenda mbio,
kuharibika mapafu, kuumwa chini ya kitovu na kupata saratani ya tumbo
la uzazi. Pia husababisha mzunguko wa hedhi kubadilika na mara nyingine
husababisha kutokuzaa kabisa,” alisema.
Aliwataka wana vyuo hao kutumia njia za asili kuzuia mimba na kuepuka matumizi ya vidhibiti mimba.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment