Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAFANYAKAZI wa Chama Kilele cha Wakulima wa Tumbaku Tanzania
(Apex), wamemtaka Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG)
kuweka hadharani taarifa ya ukaguzi wa chama hicho kutokana na kuibuka
madai kuwa kimefuja sh bilioni 16.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Mashambani na Kilimo
Tanzania (TPAWU) – Apex, Leonard Maganga, alisema wafanyakazi hao
wanaomba ripoti hiyo ili kuwaondolea hofu inayowakabili juu ya hatima
ya chama hicho kutokana na Bunge lililopita kutaka kifutwe kwa
kinachodaiwa kuwa na ubadhirifu.
“Hadi sasa tuna takribani miezi tisa tangu ufanyike ukaguzi ofisini
kwetu juu ya tuhuma na madai yaliyoorodheshwa na wabunge juu ya Apex,
lakini hakuna mrejesho… tunataka kujua hatima ili wafanyakazi tuwe na
uamuzi,” alisema Maganga.
Katika ufafanuzi wake, mwenyekiti huyo alisema wafanyakazi wa chama
hicho wanashangazwa na mswada wa Waziri wa Chakula la Ushirika,
Christopher Chiza, kukifuta wakati kuna vyama kikiwemo
kinachowaunganisha wanunuzi wa zao hilo (ATTT) ni chanzo cha kumdhulumu
mkulima pato lake.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment