Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KAMPUNI ya Tumbaku Tanzania (TLTC) imekarabati moja ya magari manne
ya zimamoto mkoani Morogoro kwa gharama ya sh milioni 7.8 ili kusaidia
idara hiyo kuboresha huduma zake.
Akikabidhi gari hilo lililokarabatiwa mjini Morogoro jana, Mkurugenzi
wa Sheria na Uhusiano wa TLTC, Richard Sinamtwa, alisema kampuni
iliamua kukarabati gari hilo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali
kujihami na majanga ya moto mkoani humo.
“Sisi kama moja ya jamii na raia wema wa Tanzania, tuliona kuwa kwa
kukarabati gari hili tunaiunga mkono serikali kupitia ushirikiano wa
serikali na taasisi binafsi katika uboreshaji wa huduma za zimamoto,”
alisema.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment