Home » » Mtaka ataka jamii kusaidia wenye uhitaji

Mtaka ataka jamii kusaidia wenye uhitaji

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mtaka ataka jamii kusaidia wenye uhitajiMKUU wa Wilaya (DC) ya Mvomero, Anthony Mtaka, ameitaka jamii kubadilika na kuwasaidia watu wenye kuhitaji misaada mbalimbali badala ya kujinufaisha wenyewe kwa mambo yasiyo na tija.
Mtaka alitoa kauli hiyo hivi karibuni alipokuwa akifungua mkutano wa kutathmini Mradi wa Tuamke Sasa wilayani humo ulioandaliwa na asasi ya kiraia inayojishughulisha na utoaji elimu ya uraia na masuala ya kijamii (Tacci).
Alisema vijana na wananchi wa sasa hawawajibiki ipasavyo na badala yake wanailalamikia serikali wakidai haijafanya lolote la maana wakati wao wangeweza kuwa chanzo cha mafanikio.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa